Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Mbeya Joseph Mbilinyi aahirisha kuhamishia biashara zake South Africa ili kumpa nafasi Rais mpya

View attachment 1753657

Hii ndio Taarifa yake mpya aliyoisambaza kwa Umma, kwamba ameamua kuahirisha mpango wake wa kuhamishia biashara zake nje ya nchi baada ya Rais mpya Samia Suluhu kuonyesha mwanga wa kujali wawekezaji.

Sugu tayari alishapata ofa ya kupewa maeneo ya kuwekeza kwenye nchi tatu za Africa ikiwemo Zambia, Malawi na South Africa, hata hivyo ameahirisha mpango huo baada ya kusikia maneno kutoka kwa Rais mpya aliyesisitiza wawekezaji kutendewa haki .

Sasa tuendelee kusikilizia kama yanayosemwa na Mh Rais ndio yatakayojiri.
Bilionea kama Bilionea.
 
sugu hana uwezo kuhamishia biashara south hata siku moja, hata uwezo wa k u jenga hotel nyingine kama ile hana. mikopo ya ubungeni ambao sasahivi hana ndio ilimwinua, hana hela kiufupi, asitishe watu.
 
Kwa nini asiendelee kuwekeza huko alikopania kuwekeza?

Kwa sababu katika jinsi ya kawaida sio kwamba angeibeba hiyo hoteli na kuihamishia huko alipokutaja...
 
sugu hana uwezo kuhamishia biashara south hata siku moja, hata uwezo wa k u jenga hotel nyingine kama ile hana. mikopo ya ubungeni ambao sasahivi hana ndio ilimwinua, hana hela kiufupi, asitishe watu.
Usiumie mkuu
 
Usiumie mkuu
siumii, namfahamu. tulikuwa tunaomboleza naye kipindi kile wanataka kubomoa hotel kisa ipo kwenye mkondo wa chanzo cha maji, tukijua amekopa mikopo atafanyeje ndugu yetu. atulie wenye hela waongee yeye bado anadanga.
 
Sugu Pesa zake kazipatia kwenye Mshahara na Mikopo ya bungeni hivyo ni vyema awekeze ndani maana italeta mzunguko wa fedha mitaani kuliko kupeleka nje ya nchi.. kwanza ndie mpinzani pakee anayependwa na ccm maana na viongozi pia... even aliyekuwa Raisi wa Awamu ya 5
 
Mama mitano tena atake asitake

Alisikika mlevi mmoja akiwa amepata kachasa akimsifia jocye banda enzi hizo
 
Hii ndio Taarifa yake mpya aliyoisambaza kwa Umma, kwamba ameamua kuahirisha mpango wake wa kuhamishia biashara zake nje ya nchi baada ya Rais mpya Samia Suluhu kuonyesha mwanga wa kujali wawekezaji.

Sugu tayari alishapata ofa ya kupewa maeneo ya kuwekeza kwenye nchi tatu za Africa ikiwemo Zambia, Malawi na South Africa, hata hivyo ameahirisha mpango huo baada ya kusikia maneno kutoka kwa Rais mpya aliyesisitiza wawekezaji kutendewa haki .

Sasa tuendelee kusikilizia kama yanayosemwa na Mh Rais ndio yatakayojiri.
Acheni siasa za kiki nyie nyumbu. Ni uonevu gani serikali ilifanya dhidi yake? Uonevu pekee ambao ulikuwa mbioni kufanyika, maraehemu JPM aliingilia kati ukaisha.

Nilimsikia bungeni siku moja akiilaumu serikali kudhibiti posho na safari kwamba hatua hiyo iliathiri sekta ndogo ya hoteli na yeye akiwa mdau. Pia siku ile aliilaumu pia serikali kwa kusitisha warsha na makongamano kwenye kumbi binafsi pale ambapo kuna kumbi za umm kuwa kunadhoofisha sekta!

Huyu mwamba namkubali sana kwenye harakati za mziki. Ila kwenye siasa huwa sioni kama anatofautiana sana na nyumbu wengine. Mwambieni aache kiki. Huko Malawi anakotaka kuenda nako serikali imeamka na "wawekezaji wanaotaka kudekezwa" nao wameanza kulialia.

Viva JPM
 
Sema Viva Hayati
 
Back
Top Bottom