Mfanyabiashara Ramadhan Hamis Ntunzwe, adai TRA hawajatekeleza agizo la Rais. Je, Kamishna Mkuu TRA afukuzwe kazi na Yono ifilisiwe mali zake?

Hajalipwa mpaka leo,analalamika sana jaman,ila kuna watu watafutwa kazi kwa jambo lake likifwatiliwa vzr.
 
Jamaa anauwezo mkubwa sana kujieleza.Nimemsilikiza kwa zaidi ya saa moja clip yake.Elimu ya ujuzi ni ziada tunazaliwa na kipaji.TRA wakae mkao wa kula ni aibu na fedheha sana zama hizi za JPM, maagizo ya JPM watu wanafanya mzaha wa ajabu!? Kama huyu aliepata bahati suala lake kupata baraka na maagizo Raisi, PM anasumbuliwa vile iweje makabwela wenzangu wa Tuangozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nadhani kunashida kubwa sasa hivi ndani ya serikari!
Maafsa wengi sana hawajari saivi.
 
Nimesikiliza clip ya jamaa. Sijasikia upande wa pili. Lakini jamaa yuko consistent na maelezo yake. Ambayo inaonesha ukweli wa anachoongea. Kwa historia mbaya ya TRA, atakuwa anasema ukweli.

 
HABARI YA KUSIKITISHA SANA TENA SANA, KATIKA MAISHA YANGU SIJAFIKIRIA KAMA KUNA WATU WANA ROHO MBAYA NA NGUMU KIASI HICHI KUWAFANYIA BINAADAMU WENZAO, HABARI YA HUYU MZEE RAMADHAN INASIKITISHA SANA, KAMA MAMBO YAPO HIVI, BASI TUSAHAU KABISA KAMA KUNA KITU KINACHOITWA MAENDELEO KWA AJILI YA NCHI YETU.
 
Huyu bwana Ramadhani ndio Yule mfanyabiashara ambae rais aliagiza alipwe na kwa maelezo haya inaonekana hajalipwa mpaka Leo.
Hapa sasa ndio hawa TRA wanaonyesha wananguvu kuliko rais kwamba maagizo ya rais kwao sichochote.
Kuna Kitu wanamtafuta Magufuli atakapoanza kula nao Sahani Moja Tutaona wanatia huruma kwa wananchi tuwatetee.
TRA mmeshamsababishia baba wa Watu kifo cha Dada yake, mkewe kaugua kichaa kwasababu yenu, hamuwezi rudisha uhai wa ndugu Zake basi mlipeni fedha anazodai walau apunhuze machungu nalo hamtaki? Kuweni basi hata na utu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karma itafanya kazi

Mimi katika kazi zangu nilikumbana na kizingiti cha makonda, yote nilimwachia Mungu atamlipa huyu Paul M
 
Inasikitisha sana, ila Kuna udhaifu nimeuona kwenye uongozi wote hivi rais au pm unatoaje tamko au amri alafu hufuatilii kama ilitekelezwa au laa?
Japo una majukumu mengi kitaifa ila swala kama hili ulitakiwa ulitilue uzito sana kwani tra sio wageni kwenu,
Au mlitaka msikie huyu mzee kauliwa au kafa?
HAPA KWA KIFUPI TRA, KUANZIA KAMISHNA MKUU, NAIBU NA HAO WAANDAMIZI NA WALIOHUSIKA KWENYE MAAMUZI WAFUKUZWE KAZI NA WAFUNGWE hata wakiachwa MUNGU atajidhihirisha kwa huyu mzee tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…