DOKEZO Mfanyabiashara wa Magari, Gideon Mlokozi Mashankara amepotea

DOKEZO Mfanyabiashara wa Magari, Gideon Mlokozi Mashankara amepotea

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii habari ni ya siku nyingi kidogo mwanzo wa mwezi hivyo edit habari ili kutoa mkanganyiko "amepotea leo siku ya 7".

Weka na picha pia mkuu isaidie watu kumtambua.
Mtu mwenye akili timamu anaelewa vizuri tu kama taarifa amecopy kutoka kwa ndugu na ameisambaza hapa.

Ukipata mkanganyiko ndio ujijuwe huna akili.
 
Ili kukabiliana na huu utekaji wa kikosi kazi ambacho kipo chang'ombe Kwa mujibu wa hotuba ya mh mbowe,serikali inatakiwa ilegeze masharti ya umiliki wa siraha kama ilivyo marekani ili tuwashughulikie Hawa wahuni wanaojifanya hawajulikani wakati wanajulikana na niwajingawajinga ambao uwezo wao wa kuchanganua mambo ni sifuri.
Sasa kila mtu akimiliki silaha si itakuwa ni suicide missions tu kila uchao. Maana ishu inakuwa sio kutekwa tena ni kupigwa njugu na wasiojulikana unaachwa ufie hapo hapo getini kwako.
 
Upole una faida na hasara zake. Mfano hapo hata kama si polisi hakuna raia waliohoji mnaangalia tu mwenzenu akipotea.
Hili nalo ni shida imgine hadi leo ndio taairifa zinasambaa wakati ilitakiwa usiku huo huo ziwe viral.

Watu wqnq simu na mitandao kwa ajili ya mpira wa yanga tu na kujadili mapenzi.
 
Anaitwa GIDEON MLOKOZI MASHANKARA ana umri wa miaka 30,mkazi wa Tabata Segerea,

Kazi yake ni mfanyabiashara wa kuuza magari lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa.

Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa jeshi la Polisi siku ya Ijumaa ya tarehe 02 August 2024 majira ya Saa 2 :00 usiku.

Akiwa katika ofisi ya magari ya rafiki yake inayojulikana kama RAPHAEL STAR iliyopo maeneo ya Segerea Stand.

Watu hao waliojitambulisha kama askari wa Jeshi la polisi walikuwa watano,walivamia ofisi hiyo wakiwa wamevalia kiraia na kumuweka Chini ya ulinzi.

Ndipo alipowahoji waoneshe vitambulisho lakini wakakaidi na kudai wanampeleka kituo cha polisi Tabata,atajua huko huko.

Walitumia nguvu na kumfunga pingu kisha wakamuingiza kwenye gari walilokuja nalo aina ya Landcruiser hardtop, ikiwa haina namba

Lakini mashuhuda waliokuwa nje ya ofisi wanasema,gari hilo halikuwa na namba kwa nyuma ila kwa mbele liliandikwa "STL" tu.

Gari hilo halikuelekea Kituo cha polisi Tabata kama walivosema bali lilielekea njia ya kwenda kinyerezi.

Familia ilianza juhudi za kumtafuta vituo vyote vya Polisi Jijini Dar es saalam bila mafanikio

Tulianza kituo cha polisi Tabata, tukaambiwa hayupo na hawana taarifa zake,Tukaenda kituo cha polisi cha Staki Shari,Kinyerezi na Buguruni pia hawakuwa na taarifa zake

Kesho yake asubuhi tuliendelea na vituo vingine tulianzia Central, Oysterbay na vituo vyote bila Mafanikio

Tumezunguka Hospitali zote jijini Dar es saalam na vyumba vya kuhifadhia maiti "Mortuary" bila Mafanikio.

Tulifungua taarifa kituo cha Polisi cha Staki Shari na kupewa RB namba STK/RB/6642/024

Baada ya siku ya tano bila Mafanikio tumeenda Central polisi kufungua jalada la Uchunguz,tumeambiwa upelelezi unaendelea.

Kwa niaba ya Familia tunaomba mtu yoyote mwenye taarifa kuhusu ndugu yetu awasiliane na Baba yake GIDEON kwa namba 0786878133 au kwa namba ya rafiki yake ambayo ni 0624497811

Asante sana.
Nadhani tuwe na sheria ya kumiliki silaha ya lazima kwa kila raia. Sababu ni kuwa inawezekana kuna organized crimes ambapo kuna mafia group watu wakidhulumiana basi kinatumwa kikundi kumteka mtu
 
Back
Top Bottom