Hii ni moja ya atuwa kubwa Sana katika kumkomboa mfanyakazi na kuipa thamani KAZI yake. Mimi nataka kuamini SASA tutaelewana tena Sana. Ikumbukwe Kwa waajiri ni msumari wa Moto katika kidonda. Why SASA badala yakumtambuwa kama muwajiri ndie mlipa Kodi SASA serikali inamtambua muajiriwa kama mlipa Kodi na kuweza kuthamini KAZI yake Kwa kumrudishia kile amelilipa zaidi na kumrudishia muhusika pitia Tin number yake.
Ikumbukwe Kwa SASA waajiri wanajuwa au wanajimilikisha return za ziada ya Kodi pasipo warudishia wafanyakazi kwa kuwa tu pesa walilipa wao.
Mfumo mpya utaleta uwazi na uwajibikaji na huenda mfanyakazi kwa mara ya kwanza ataona faida ya kodi yake kwa kurudishiwa ziada yake na pia kupata exemption ya serikali. Ikumbukwe waajiri wanaifaidi hii exemption kwa kulalia mgongoni Kwa wafanyakazi Jambo sio Sawa.
Upande wa pili ni hatari maana sasa huenda mishara ya watu itakuwa ikijulikana na TRA jambo makampuni mengi yasingependa ijulikane. Hasa wale wanalamba mishara minono.
Kuna kila dalili huenda payee mara mfumo huu utaanza kutumika itaongezeka sana au kupungua ila kwa njia za udanganyifu.