Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Utaratibu mzuri na mwenye faida na mchungu kwa mfanyakazi.... Tunakoenda watasema wanafunzi waanze kupatiwa TIN mapema....Tunakoenda pia. Wanachi Wote Utahitaji kuwa na TIN kupata huduma kadhaa.... Wanaforce kuongeza Wigo WA kodi
Duuh, asante mkuu
 
Ni vizuri kujizoesha kuwa na mawazo positive...SIO KILA KITU ni kuwazia negative
Ninavyo fahamu, huo ni utambulisho tu kuwa mfanyakazi ndiye mlipa kodi na sio taasisi/kampuni kwa kuwa wewe ndiye unakatwa mshahara wako.

Lakini pia, ikatokea kukawa na tax exemption mfanyakazi ataweza kunufaika kwani sasa ataweza kuthibitisha kuwa, yeye ni miongoni mwa walipa kodi wazuri. Kumbuka kuna wafanyakazi wanalipa kodi ya mshahara sawa au zaidi ya baadhi ya wamiliki wa maduka makubwa ila kwa sasa hawatambuliki, hivyo ikitokea tax exemption hawawezi kupata msamaha..

Mwisho; itasaidia serikali ukusanyaji wa mapato kwani wakiona mtu fulani hajatoa kodi ya mshahara, itabidi taasisi/shirika husika liulizwe ili litoe maelezo

Kwanini hawatambuliki wakati record zao zipo tena kwa majina yao kamili na kila mfanyakazi ana namba ya ajira yake ambazo ziko TRA. Hivi unaona una akili sawasawa kusema record za wafanyakazi wanaolipa kodi hazipo, unamaanisha nini. Zinakosekanaje kama hata mashirika ya pension yana record ya mfanyakazi tangu alipoajiriwa ikiwa wao wanalipwa pesa ndogo sana ukilinganisha na TRA. Kinashindikana nini kutumia kumbukumbu zilizopo kujuwa wafanyakazi wanalipa kodi kiasi gani.
 
Kuna taarifa inasambazwa kwa video clip na magazetini ikiwa imetolewa na TRA kuwataka waajiliwa wote kuwa na TIN. Ni taarifa ambayo naona kama inatokana na uongozi wa TRA wenye mapungufu ya hekima. Kwanza imeletwa ikiwa na kikomo (ultimatum) wakiamini wanayo nguvu hiyo ya kuwapa ultimatum waajiliwa wote. Pili imetolewa utadhani ni jambo la dharula. Tatu imetolewa kwa lugha ya hovyo, isiyo na uungwana pamoja na tishio la kuzuia mshahara wa mwajiliwa.

Naomba TRA wasijitwishe madaraka yasiyo yao. Mwajiliwa yeyote hajawahi kuwa na mkataba wa aina hiyo na TRA. Kama TRA wanaleta utaratibu mpya, wanatakiwa wawe waungwana (reasonable). Walete taarifa ya kiungwana na siyo kutishia wakati hakuna mwenye makosa. Labda wanaiga lugha za viongozi wanaomiliki vyombo vya dola. TRA hana nguvu ya aina hiyo na ni makosa kutishia watu wasio na mkataba wa aina hiyo.
 
Google hii subject ya ( wanaosamehewa Kodi ya paye Tanzania) utapata majibu
Ni suala la muda mrefu hata bungeni nakumbuka upendo pendeza alihoji hili suala akajibiwa kiuni na waziri mpango
Mkuu binafsi nimekuelewa.
 
Back
Top Bottom