Mwandishi wa habari na Mtangazaji maarufu Nchini, Rahabu Fredy aliyekuwa mhariri katika kituo cha habari cha Azam Media, amefariki dunia leo April 5, 2025 akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Rahabu ambaye alikuwa mke wa aliyekuwa mtangazaji mahiri, marehemu Fred Fidelis almaarufu Fredwaa, alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Rahabu na Fredwaa walipata umaarufu mkubwa enzi za uhai wao wakifanya kazi katika Kituo cha Radio Free Africa jijini Mwanza kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam.