TANZIA Mfanyakazi wa Azam Tv, Rahabu Fungo amefariki Dunia

TANZIA Mfanyakazi wa Azam Tv, Rahabu Fungo amefariki Dunia

TANZIA: Uongozi wa kampuni ya Azam Media Limited, unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wake, Rahab Fred Fungo, aliyekuwa Mhariri Mkuu Msaidizi kwenye Idara ya Habari na Matukio.

View attachment 3294329
Rahab amefariki dunia Aprili 5, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Azam Media Limited inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza kifo cha mpendwa wetu.
rahab fred pumzika kwa amani
 
Sikujua aliishiaga wapi ila nilivyoskia taarifa hizi sauti yake inazunguka akilini
 
Nimeanza kumsikia wakati redio free Africa,, Mbeya walikuwa wanakata kutoka station kuu mwanza tunaanza kusikia redio free Africa Mbeya,,, R.I P
 
Back
Top Bottom