TANZIA Mfanyakazi wa CRDB afariki akifanya mazoezi Daraja la Tanzanite

TANZIA Mfanyakazi wa CRDB afariki akifanya mazoezi Daraja la Tanzanite

Muhimu sana kucheki pressure. Kufanya jogging sio jambo la lazima kwa kila mtu kulifanya muda mwingine ni vema kufanya mazoezi ya viungoa madogo madogo kama kustrech then unafocus na maswala ya chakula tu. Muhimu ni kubalance diet yako mazoezi si lazima kukimbia hata kutembea ni mazoezi mazuri sana.
Sasa mbona hata wenye pressure wanashauriwa kufanya mazoez?
 
Mfanyakazi wa benki ya CRDB, Stanley Josiah amefariki dunia akiwa anafanya mazoezi kwenye Daraja la Tanzanite.

Taarifa za kifo chake hicho zimethibitishwa leo Jumamosi Juni 14,2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano

Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, alipozungumza na Mwananchi Didital.

Tully amesema mpaka mauti yanamkuta, Josiah alikuwa mkuu wa kitengo cha operesheni za mikopo Benki ya CRDB.

"Benki imepoteza mtu mahiri sana hivyo menejimenti na wafanyakazi inaungana na familia yake katika safari hii ya mwisho," amesema Mwambapa ambaye ameeleza kuwa msiba upo nyumbani kwa marehemu, Tabata Kinyerezi.

"Benki inashirikiana na familia tangu taarifa ya ajali ilipotokea hadi sasa kufanya maandalizi yote muhimu hadi siku ya kumpumzisha mwenzetu kwa taratibu tulizojiwekea kama benki," amesema na kuongeza kuwa, mwili wa marehemu unatarajiwa kupumzishwa Jumanne ijayo Juni 17, 2025 nyumbani kwako huko mkoani Mbeya.

Hata hivyo taarifa ambazo Mwananchi imezipata, zinasema alifika asubuhi mapema ofisini na kuacha gari yake ofisini kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi ya kukimbia.

Chanzo hicho cha habari kinasema, mara nyingi hufanya hivyo kila siku asubuhi.
View attachment 3368481
RIP bro
 
Acheni ufala na uzandeki, habari inasema amekufa akiwa anafanya mazoezi, sio amekufa kwa sababu yakufanya mazoezi, unajua wabongo mna mambo yakimaku sana, mtu anaeza kufa popote huyu kafa akiwa mazoezini wewe unaeza kufa ukiwa kifuani mwa mshangazi, habari kusema ooh alikua na presha nk ni ushamba maana kwa taarifa yenu mazoezi yanapunguza presha na sio kuongeza...
Mungu amlaze mahala pema mwana mazoezi mwenzangu bora yeye kafa kwenye mazoezi sio wewe unaeeza kufa ukiwa unatype kwenye simu kuomba mchepuko gemu
 
Nilichogundua huku Jf watu wengi mna comment vitu msivovijua!
Acheni ujuaji!!
Kila mtu anassugest chanzo chake cha kifo !mara heart attack mara bla blaaa!!
Yani kila mtu anajiandikia anachokijua!!
 
Kuna wadau mna comment kama kuku walio katwa vichwa,alikuwa anafanya mazoezi mlevi kam gonga na gari. Kama mmesoma vizuri ni utaratibu wake wa kila siku kufanya mazoezi asipate cardiac arrest alipo anza aje apate amesha zoea mazoezi?
 
Kuna wadau mna comment kama kuku walio katwa vichwa,alikuwa anafanya mazoezi mlevi kam gonga na gari. Kama mmesoma vizuri ni utaratibu wake wa kila siku kufanya mazoezi asipate cardiac arrest alipo anza aje apate amesha zoea mazoezi?
So sad, umakini unahitajika barabarani wakati wa mazoezi kwani barabara ina mengi walevi, ma'learner, wenyemawazo n.k

Ombi langu kwa wanamazoezi wote wanaotumia barabara, jali kwanza mazingira ya usalama wa barabara ufanyapo mazoezi yako.
 
Kwani hana jina?
Kwani jina pekee linaweza kumtambulisha mtu?
Hakuna ubaya hapo mkuu, katika uandishi ni muhimu sana kuzingatia haya:-

1. Nini/Nani?
2. Lini?
3. Wapi?
4. Kwanini?
5. Kwa namna gani?
 
Back
Top Bottom