Mfanyakazi wa ndani akamatwa akituhumiwa kumuua mama, wanaye wawili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Shadrack Kapanga (34) kwa tuhuma za mauaji ya mama na watoto wake wawili eneo la Masaki mtaa wa Maryknol.

Kapanga ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani alikamatwa jana Ijumaa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya kuwaua Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 12, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.

“Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni simu za marehemu, televisheni, king’amuzi cha DSTV na rimoti,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Muliro ameeleza kuwa upelelezi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la mauaji Juni 9, 2021 baada ya kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

“ Baada ya kuwaua aliwafungia ndani na kutoroka. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kujua sababu za msingi za mauaji hayo na mara utakapokamilika mhusika/wahusika watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” inaeleza.

Soma pia:

1). Familia ya marehemu Joe Mutaboyerwa yavamiwa; mama na watoto wawili wauawa

Mwananchi
 
Aisee.

Mimi ni muumini wa death sentence. Mtu kafanya ujinga kama huo hatuna sababu ya kuchanga na kumlipia kula chakula gerezani, anatakiwa kunyongwa.

Kamaliza kizazi cha mtu kwa ujinga wake.
Tanzania hakunaga kunyongwa wewe.

Death sentence zinatoka lakin mpaka raisi asaini hati ya kifo.
Nasikia tangu Nyerere ang'atuke hakuna raisi aliyethubutu.

Wafungwa wanakula maisha tu.

Halafu unajua ukihukumiwa kifo hufanyi kazi yoyote gerezani? Yani wewe ni kula good time mpaka upate natural death.
 
Halafu cha kushangaza utasikia upelelezi haujakamilika kesi inacheleweshwa mara sijui kitu gani bado, mpaka miaka 4 tayari machungu ya kupoteza wapendwa wao yanatoweka, utasikia aliua bila kukusudia.

Nimeangalia zile picha zao wakiwa hai yaani Inasikitisha mno.

Hizi Sheria zetu za Demokrasi ni mtihani kwakweli. Kwetu Arabuni akiua na yeye lazima auliwe, ili kubalance maumivu.

Kamaa tadinu tudanu..Utakavyofanya ndiyo unakanyo fanyiwa.
 
Tanzania hakunaga kunyongwa wewe.
Death sentence zinatoka lakin mpaka raisi asaini hati ya kifo.
Nasikia tangu Nyerere ang'atuke hakuna raisi aliyethubutu.
Wafungwa wanakula maisha tu.

Halafu unajua ukihukumiwa kifo hufanyi kazi yoyote gerezani? Yani wewe ni kula good time mpaka upate natural death.
Hii sheria ya mpaka Raisi atie saini ndo inatuchelewesha sana tungekuwa na wabunge waerevu wangependekeza Saini ya kunyongwa ibadilike awe anasaini ata Mkuu wa Magereza wa nchi ssa jitu kama ilo likihukumiwa kunyongwa litakua halina cha kupoteza litaenda kula bata tu uko gerezani INASIKITISHA SANA
 
Tanzania hakunaga kunyongwa wewe.
Death sentence zinatoka lakin mpaka raisi asaini hati ya kifo.
Nasikia tangu Nyerere ang'atuke hakuna raisi aliyethubutu.
Wafungwa wanakula maisha tu.

Halafu unajua ukihukumiwa kifo hufanyi kazi yoyote gerezani? Yani wewe ni kula good time mpaka upate natural death.
Za kusikia changanya na zako. Rtd president hajanyonga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Shadrack Kapanga (34) kwa tuhuma za mauaji ya mama na watoto wake wawili eneo la Masaki mtaa wa Maryknol.

Kapanga ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani alikamatwa jana Ijumaa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya kuwaua Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Juni 12, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.

“Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni simu za marehemu, televisheni, king’amuzi cha DSTV na rimoti,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Muliro ameeleza kuwa upelelezi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la mauaji Juni 9, 2021 baada ya kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

“ Baada ya kuwaua aliwafungia ndani na kutoroka. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kujua sababu za msingi za mauaji hayo na mara utakapokamilika mhusika/wahusika watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” inaeleza.

Mwananchi
Jina sahihi ni Mutayoberwa, sio Mutaboyerwa,
Kihaya hicho
 
Ina maana kwenye hiyo nyumba alikuwa anakaa yeye na hao ndugu tu?
 
Back
Top Bottom