mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
Mnamo Mei 2019, Adeleye, mama aliyekuwa mfanyakazi wa kulea watoto mwenye umri wa miaka 73 kutoka nchini Nigeria, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela huko Prince George’s County, Maryland, Marekani. Adeleye alipatikana na hatia ya mauaji ya second degree muder na unyanyasaji wa mtoto wa daraja la kwanza, na unyanyasaji wa mtoto wa daraja la pili, kufuatia kifo cha Enita Salub mwenye umri wa miezi minane mwaka 2016.
Ipo hivi.
Picha za kamera ya ndani ya nyumba za Oktoba 24, 2016, zilionyesha mtoto huyo akivuta nguo ya Adeleye ili kumwamsha alipokuwa amelala kwenye sofa . Kwa mujibu wa waendesha mashtaka na video ya kamera ya usalama, Oluremi Adeleye alikuwa amelala kwenye sofa wakati mtoto huyo akilia na kumsumbua.
Kamera ilimrekodi mtoto huyo akiwa kwenye kigari cha watoto, akilia, akivuta nguo ya Adeleye na kumpiga mguuni akijaribu kumwamsha. Baada ya kuamka, Adeleye alijaribu kwanza kumlisha mtoto kwa chupa kama kawaida, lakini mtoto alikataa.
Kwa sababu ya kuchoshwa na kilio na kukataa kwa mtoto kunywa, Adeleye alifungua kifuniko cha chupa na kumimina maziwa moja kwa moja kwenye mdomowa mtoto huyo.
Alimimina karibu mm250 za maziwa moja kwa moja kwenye koo la mtoto huyo ndani ya muda wa chini ya sekunde 30.
Kiasi hicho kikubwa cha maziwa kilimfanya mtoto ashindwe kupumua na mwili wake kulegea. Uchunguzi wa kitabibu baada ya kifo ulionyesha kuwa chanzo cha kifo kilikuwa kukosa hewa. Waendesha mashtaka walisema kwa maana fulani mtoto huyo “alizama” kwenye maziwa.
Wakati wa kesi yake iliyosikilizwa na jaji bila jopo la majaji, Adeleye alitoa ushahidi kwamba hakuwa na nia ya kumdhuru mtoto. Yeye pamoja na mashahidi wa upande wake wa utetezi walidai kuwa alikuwa akifanya kile kinachojulikana kama “cup-feeding”, desturi ya jadi ya Nigeria ya kuhakikisha mtoto anapata chakula hata anapokataa kula.
Hata hivyo, jaji alikataa hoja hiyo ya kitamaduni kuwa haiwezi kutumika kama sababu ya kuhalalisha unyanyasaji mkubwa wa mtoto. Hatimaye, Adeleye alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 15 jela, kikifuatiwa na miaka mitano ya uangalizi maalumu baada ya kutoka gerezani.
NB: kuweni makini na mnaowaajiri kama waangalizi wa watoto wenu majumbani