Mfanyakazi wa ndani auawa Uarabuni na mwili wake kutupwa chini ya gari

Mfanyakazi wa ndani auawa Uarabuni na mwili wake kutupwa chini ya gari

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Mfanyakazi wa ndani mwenye asili ya Kiafrika Faustina Tay aliyekuwa akifanya kazi nchini Lebanon amekutwa amefariki baada ya kutuma ujumbe kuwa alikuwa akinyanyaswa

Mfanyakazi huyo raia wa miaka 18 kutoka Ghana kabla ya kifo chake alituma ujumbemfupi kwa wanaharakati wa kutetea wafanyakazi wa ndani, na masaa 18 baadae mwili wake ukakutwa chini ya Gari, uchunguzi unaonyesha kuwa alisukumwa juu ya ghorofa na kubamiza kichwa

Nchi ya Lebanon ina wafanyakazi wa ndani wapatao 250,000 na inakadiriwa wafanyakazi wawili hufa kila wiki lakini Serikali haifuatilii mauaji hayo

Chanzo: Al Jazeera
The desperate final days of a domestic worker in Lebanon
b1f7cf318dd54e94a4735d4da1046d97_18.jpg

Faustina Tay akielezea mateso yake kwa njia ya video


98a789a011fa4a8995972a0c803db1ec_18.jpg

Faustina Tay siku aliyowasili Lebanon akitokea Ghana
 
Msisahau yule mama wa kibongo aliyepiga housegirl mpaka akaua,
Hakuna cha mwarabu hapa, binadamu ni walewale

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo nimesoma wapo 250,000 na kila wiki wanakufa wawili, Watanzania hatuna roho mbaya hivi, mbaya zaidi Serikali haifanyi chochote, Huyo mama wa Kibongo tuliona kabisa alivyochukuliwa hatua
 
Msisahau yule mama wa kibongo aliyepiga housegirl mpaka akaua,
Hakuna cha mwarabu hapa, binadamu ni walewale

Sent using Jamii Forums mobile app
Yule mama sasa hivi yupo wapi?! Tofauti ni kuwa huko Uarabuni muuaji hafanywi chochote kwasababu kaua black person.

Mnajaribu ku justify huu ukatili kwa kusema mara US au Europe haya mambo pia yanatokea ila tofauti ni kuwa huko mhalifu anashughulikiwa ila huko Uarabuni muuaji hafanywi chochote kwasababu kaua black person.
 
Kuna mmoja nilisoma story yake kwenye gazeti. Anatoka Nigeria, baada ya kufanya kazi miezi 24 Dubai aliweza kurudisha nauli iliyompeleka na akafungua mgahawa kwao. Sasa ni boss kwenye mgahawa wake.
Hizi stori ndio zinafanya waende huko pamoja na wengi wao kuuawa. Ukija kuangalia huo mgahawa utakuta hata waliobaki hapo kwao wanaweza kuanzisha.
 
Mbali na yote hayo wasichana tumekuwa hatujifunzi kwani si ajabu limetokea hili lakini yupo mwingine anasubiria Corona iishe aende akafanye hizo hizo kazi za ndani.
Watu wapo desperate sana, mi siwalaumu, nawalaumu watesaji
 
Back
Top Bottom