Mfanyakazi wa Serikali akisafiri nje analipwa zaidi ya dola 350 Kwa siku sawa na zaidi ya Tsh 400,000

Mfanyakazi wa Serikali akisafiri nje analipwa zaidi ya dola 350 Kwa siku sawa na zaidi ya Tsh 400,000

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nilikuwa wa kwanza kushtuka kusikia fedha walizolipwa wafanyakazi wa MSD, lakini Baada ya kufanya utafiti nimebaini Kila mfanyakazi wa Serikali akisafiri nje ulipwa zaidi ya dola 350. Kabla ya kulalamikia MSD ni vyema tukafahamu sheria inayotumika kufanya malipo.

Kwa viongozi wakuu wa Nchi inaweza ikawa wanalipwa mara tatu zaidi ya kiwango nilichotaja. Hii kibongo bongo inaweza kuwa fedha nyingi lakini huko nje ambapo hotel Kwa siku ni zaidi ya dola 100 Bado ni fedha ndogo.

Lakini Kwa Mtanzania anayefanya kazi shirika la Kimataifa akiwa nje ya Nchi husika analipwa about 1000 USD sawa na zaidi ya milioni mbili na laki mbili Kwa siku Moja.

Kwa wale tuliosafiri nje tukiongeza na maujuzi ya kusoma soma taratibu za serikali tunaweza kubalance discussion kama hizi zinazoendelea ambazo unabaini magazeti yote na vyombo vya habari hakuna kilichoweza kufanya utafiti au kuhoji ulipaji serikalini upoje?

Mimi Naamini serikalini watu wanaiba kupitia sheria zilizopo zinazotamka Haki. Kama hakuna sheria inayotoa limit ya jambo fulani ni vigumu kulifanya Liwe kosa Hadi pale litakapofanywa kosa.
 
Kuna mzee wangu alikuwa akisafiri..akirudi anabakiwa na change mpka usd 10k
 
Kuna mzee wangu alikuwa akisafiri..akirudi anabakiwa na change mpka usd 10k
Hivyo hivyo mzee wa rafiki yangu alikuwa airport enzi hizo... Mimi sina tatizo na kulipana pesa za hivyo tatizo watu wa serikali yetu ni "deliverables" Pesa wanazolipana na matokeo ya kazi walizoenda kuzifanya ni sawasawa na zero.

Huwezi kufananisha serikali na sekta binafsi linapokuja suala la matokeo, kama hao walioenda china wanaweza kutuambia achievement yao ni ipi kama si vichekesho vitupu.
 
Siku 61 ni nyingi mno,je walikuwa wana assemble space shuttle au walikuwa wanahudhulia kikao cha bunge la bajeti ya Watu wa Jamhuri ya China 🇨🇳?
 
Nilikuwa wa kwanza kushtuka kusikia fedha walizolipwa wafanyakazi wa MSD, lakini Baada ya kufanya utafiti nimebaini Kila mfanyakazi wa serikali akisafiri nje ulipwa zaidi ya dola 350...
Hao wafanyakazi wanaosafiri ni wangapi kati ya wafanyakazi wa serikali zaidi ya laki tano? Na wanasafiri mara ngapi kwa mwaka?

Taarifa ni sahihi, ila utamfanya hata mwalimu wa shule ya msingi kule Namtumbo aonekane anafaidika na hizo dola 350, wakati hata nafasi ya kusafiri hana.

Pesa si ya kutisha kama nafasi wangekuwa wanapata watu mbalimbali kwa malengo yenye tija kwa taifa. Shida wanaopata ni wale wale walioko sehemu nyeti na bahati mbaya wanapewa vibali vya kusafiri na ofisi hizo hizo zinazolalamika kwenye vyombo vya habari.
 
Hivyo hivyo mzee wa rafiki yangu alikuwa airport enzi hizo... Mimi sina tatizo na kulipana pesa za hivyo tatizo watu wa serikali yetu ni "deliverables" Pesa wanazolipana na matokeo ya kazi walizoenda kuzifanya ni sawasawa na zero.

Huwezi kufananisha serikali na sekta binafsi linapokuja suala la matokeo, kama hao walioenda china wanaweza kutuambia achievement yao ni ipi kama si vichekesho vitupu.

Kwa hiyo zile kelele za CAG ilikuwa ni upepo tuu!
 
Back
Top Bottom