Mfanyakazi wa TRA akutwa amehifadhi pesa taslimu Tsh. Bilioni 7 nyumbani

Mfanyakazi wa TRA akutwa amehifadhi pesa taslimu Tsh. Bilioni 7 nyumbani

Madhara yake ndio yamezaa huu ufisadi wale watumishi waliokuwa waaminifu na wazalendo serikali iliwatupa wakawa na maisha magumu zaidi ya mbwa wengi walikufa kwa stress za kubezwa na kuchekwa si ulijifanya mnoko kipo watu hata sh elf 2 huna, matokeo yake wakajaa sana chuki na kuwapandikiza watoto wao roho za wizi na upigaji ili watoto wao wasijeishi maisha mabovu kama wao.
Kwahiyo ni halali yao kuiba !
 
Sawa Fanya mageuzi Kwa nchi Sasa Ili ufe wengine wale pesa sio unaongelea kwenye shuka unataka nani akupambanie
Mimi sijazungumzia kupambana ila nilichomaindi ni kukatisha tamaa mtu ambaye ameamua kupambana. Mimi siko kwenye position ambayo naweza kuleta impact ndio maana siwezi jihusisha na harakati kwa sasa.
 
Hongera sana Mkuu Extrovert ni wachache sana hapa Tz wenye moyo kama huo. Wengi wabinafsi, anaona yeye anajitosheleza, wengine watajijua wenyewe.

watu wanaogopa sijui kuumia, kufa. Na hiyo ndiyo hofu walishaiweka hawa serikali. Kwamba atakayekaidi, atakutana na kipigo cha mbwa mwizi. Wataua Taifa zima? Pia ujiulize, mtu anayeng'ang'ania madaraka, mpaka anaua je ni madaraka tu au kuna kingine ndani ya hayo madaraka?

Acha tuendelee kuwa keyboard warrior. Iko siku kila mtu, ataamka kwake ajikute barabarani mwenyewe, yakiwafika shingoni.
Wabongo wanapenda kuishi tu hawajali wanaishi mazingira gani ilimradi wanapumua tu. Thats completely wrong na tumekuwa tied na statements kama "Tuilinde Amani yetu"..."Amani yetu ni tunu" while kuna watu they don't give a flying fvck about hio amani as long as ya kwao yanawaendea. Ukiingia kwenye line zao wanakupoteza in a blink of a second ni vita yani ila amani inahubiriwa ili tu wao waendelee kufanya yao bila bugudha. Its more of kutiana uwoga tu ila in a real sense hakuna hio amani tunayodanganyana kuwa ipo.
 
Magufuli alinunuwa MV Kigamboni kwa 6b na haikuwahi kutoa huduma
Sawa lakini muhimu siku moja aje Dikiteta Mzalendo Muadilifu kisha akae madarakani kwa muda usiopungua miaka 30 !
Muhimu awe Mzalendo Muadilifu !
Majizi yote yashughulikiwe kikamilifu !

Kinyume cha hivyo majizi yenye kuficha bilioni 7 za tra nyumbani na majizi mengineyo yataendelea kuzalishwa kila kona !
Kila mwaka CAG anaibua madudu mapya !
Au nasema uongo ndugu zanguni ???! 😳
 

Gazeti la Raia mwema leo, Julai 10, 2024, linaeelezea utajiri wa kutisha wa mabosi wa TRA, hawa ndio wale hutuma vijana wao waje kiusumbua mtaani na kodi za Tsh. 100,000 wakati kuna watu wanakwepa kodi za trilion za pesa kwa makubaliano.

Hawa ndio wale tunaambiwa tutunze amani ili waibe na kula kwa amani, yaani ukisikia tenzi za amani yetu sababu ni hizo hapo.

Rais anasisitiza tulipe Kodi, Mwigulu anasisitiza tulipe kodi, Ila shida inakuja kwenye matumizi ya hizo kodi tunazo komaliwa tulipe na tunaambiwa kulipa kodi ni uzalendo. Na hawa watu ni kama Raisi anawaogopa sana.

Ndio maana nashangaa sana wanao jitolea mara kujenga Zahani mara shule, kwa sababu base ya kujitolea haiwezi kuwa habari kama hizi za fedha kupigwa na wengine mnambiwa wajitolee kujenga shule au Barabara au changishaneni.

Jiulize watuhumiwa wa report ya CAG wanafanywaga nini? hawakuna wanacho fanywa na sio hivyo tu bali pia husamehewa.

Hawa huwezi sikia Wakina Makala, na kampuki yake wanawazungumzia, huwezi wakuta waimba pambio humu wanazungumzia mambo kama haya. Wao wako busy na Mbowe na Lissu.

Kule Kilimanjaro kuna raia wanachangishana kulima barabara, vipi wanapo sikia habari kama hizi?
Ndio maana wanafukuzana.....mgao umeenda ndivyo sivyo
 
Sawa lakini muhimu siku moja aje Dikiteta Mzalendo Muadilifu kisha akae madarakani kwa muda usiopungua miaka 30 !
Muhimu awe Mzalendo Muadilifu !
Majizi yote yashughulikiwe kikamilifu !

Kinyume cha hivyo majizi yenye kuficha bilioni 7 za tra nyumbani na majizi mengineyo yataendelea kuzalishwa kila kona !
Kila mwaka CAG anaibua madudu mapya !
Au nasema uongo ndugu zanguni ???! 😳
Hakuna Dikteta mzalendo....ni dikiteta tu
 
Kwa sababu tuna uwezo wa kuruka viunzi vya sheria zilizopo labda !
Sheria kali kama za China ni muhimu !
Wale Wachina waliziweka zile sheria kwa sababu walijua majizi yatawakwamisha katika kupata maendeleo ya kweli na ya haraka !🙌👍
Hizi nyepesi zenyewe zinafatwa? Yaani wezi wajitungie sheria kali dhidi yao?.
Nani alitunga sheria ya kinga dhidi ya viongozi? Na juzi juzi kuna mtu aliongeza list ya viongozi wasioshtakiwa kwa jinai wanazofanya.
 
Back
Top Bottom