South Korea wanashika nafasi ya tano katika global firepower index huku Israel ikiwa ya 15.
South Korea na wao wana modified/customized versions za figter jets za kimarekani kama F-15 na F-16 kama Israel inavyofanya.
Hata Saudia , Japan, Singapore, Qatar, UAE na Taiwan wana modified versions za ndege za kimarekani. Hasa F-15 na F-16.
Mfano F-15E ya US kwa Saudi wanaita ni F-15SA(Saudi Advanced), kwa Japan wana F-15J, Singapore wana F-15SG, Qatar wana F-15QA, Taiwan wana F-15V(Viper) n.k hawa wote ni washirika wazuri wa US.
Hapo sioni maajabu lakini tu South Korea wana ballistic na cruise missiles zao za Hyunmoo series au monster missile, Mfano Hyunmoo-5 missiles zinabeba warhead yenye uzito wa ton 8 hadi 9 ni kama bunker buster maana ina penetrate kama mita 100 hivi kwenye concrete ngumu kama mwamba na wameitengeneza mahususi kulenga makao makuu ya kiuongozi ya North Korea yaliyopo chini ya ardhi.
Hilo kombora lina speed ya mach 10 wakati linakwenda kulenga target.. na lina range ya 600KM.
Hyunmoo-4 ina range ya 800KM inabeba warhead ya tani mbili.
Kwenye cruise missiles wana missiles kama Hyunmoo-3 ambayo haina tofauti sana na Tomahawk ya kimarekani ambayo sasa US wameishiwa.
Wana Hyunmoo 3C ambayo ina accurate kubwa na kwenda hadi umbali wa 1500KM, wana makombora pia ya ku launch kwa meli kama Haesong II na III.
Tuje kwenye hoja muhimu, kwanini hawa washirika wa US wananunua ndege za US na kuzi modify, ni kwa sababu ili ziendane na mazingira yao na mahitaji. Mfano Israel ili modify F-15 iweze kuendana na mazingira yake kijiografa na kimatumizi.
Na wanafanya hivi ili kuwa na silaha ambazo wanaweza kuzitumia dhidi ya maadui zao ambpo mara nyingi ni majirani au wapo kwenye ukanda mmoja.
Nachoweza kusema ni kwamba silaha nyingi za South Korea ambao ni domestic made zimetengenezwa kukabiliana na North Korea hata ukiangalia range zake na sifa zake.
Range kati ya Iran na South Korea ni kama 6500KM, Range ya Israel na Iran ni kama 1600KM au zaidi. Ndio maana Iran wana missiles nyingi za 2000KM range ambazo zinaweza ku cover Israel mahala popote.
Nachoweza kusema ni kwamba, South Korea ikiingia kwenye huu mgogoro sidhani kama kuna maajabu yeyote, na sifahamu watatumia base ipi na ndege zipi..
Namaanisha SOuth Korea anaingia kwenye mgogoro ambao hakujiandaa nao, kwa kifupi atakurupuka, atatumia silaha za EU na US kama hizo cruise missiles za kubebwa na ndege. Active personnel ni kama 569K huku reserve wakiwa 3.1 million, kiukweki wana askari wengi.
Lakini kijiografia, historia, maandalizi na aina ya silaha walizonazo huu mgogoro ni kama hauendani na maandalizi ya jeshi lao. Hayo ni mawazo yangu binafsi.
Kuhusu nuclear hawana, ndege wanazo kama 1540 huku Israel wakiwa na ndege kama 530 hivi...