Mfululizo wa ajali bila hatua kuchukuliwa ulimng'oa waziri

Mfululizo wa ajali bila hatua kuchukuliwa ulimng'oa waziri

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
Ni Mwigulu alipotumbuliwa uwaziri wa mambo ya ndani. Namnukuu hayati JPM.

"nimechoka kutoa salamu za rambirambi kwa sababu ya ajali kila siku, nimechoka, it's too much (kwa uchungu with a very serious tone). Mbaya zaidi ninayetoa ni mimi tu huku waziri akiwa anazurula bila kuchukua hatua yoyote."

Someone else, "ajali zimekuwa nyingi sana siku hizi. Lazima tujiulize tunafeli wapi??" halafu anamalizia, "hili nalo mkalitazame" inakuwa imeisha hiyo. Ni vyema Mheshimiwa Rais akaiga hii tabia ya kuchukua hatua mara moja. Mambo ya kubembelezana na wasaidizi wake yanamharibia sana.
 
Ni kweli ajali zimekuwa nyingi sana. Na hakuna juhudi za dhati kukabiliana na tatizo hili. Barabarani sio sehemu salama kabisa
Hakuna kiongozi anayejali wote wapo kimya siyo waziri wa mambo ya ndani wala IGP
 
Ni kweli ajali zimekuwa nyingi sana. Na hakuna juhudi za dhati kukabiliana na tatizo hili. Barabarani sio sehemu salama kabisa
Hatua zipi mkuu unataka? Ungependa magari yasitumike kabisa? Au iwe mwendo wa kutembea kwa miguu tu?

Ila kusema kweli tamko la Kinana limetupa kupumua sana tu mlikuwa mmetuchosha mno na rushwa zenu wakuu.

Habari ndiyo hiyo.
 
Mimi huwa najisemea kukomesha rushwa kwa traffic ni kazi rahisi sana. Yani watu wanachukua rushwa barabarani kweupe hivi kweli kwa nchi iliyo serious inashindwa kukomesha rushwa kweli? Yani tuko kwenye basi au daladala abiria wote tunajua kabisa konda ameenda kumpoza traffic.

Ni vile tu kila mmoja anakula urefu wa kamba yake. Rubishhhh
 
Back
Top Bottom