Mfumo mpya wa kutuma fedha kwa simu kuanza Julai

Tutakuwa Amna mtu wa kati hapo si unajua ukikatwa pesa yeyete ile kuna watu kama watatu wanagawana hiyo hela
SUPER DEALER hana kazi tena!
Hakuna udalali! Yaani...

Everyday is Saturday............................... šŸ˜Ž
 
Hata mimi sijaelewa!!
Huo mfumo utapunguza gharama za kutuma fedha, hapo sijaelewa gharama zitapungua vipi maana hapo wamerahisisha tuu njia ya kutuma.
Kuna jambo halieleweki hapa, watu wanatoa sababu hazina mashiko.

Hizi namba za simu zote zimesajiliwa tena kwa ganda la taifa ikiunganisha majina yako na unapoishi na kama namba ni ya mtu mwingine hauwezi kusajiliwa.

Leo eti mfumo mpya kwa majina yako, means hii techn ya sasa ni fake!.
 
Hii ni rahisi kwani database za mitandao yote zitakua kwenye mfumo kwahiyo hakuna kuingiza namba wala kuchagua mtandao, unaweka jina lililosajiliwa la mhusika, mpunga unakwenda.
Kwa hiyo hii tuliyo sajiliwa kwayo haipo kwenye mfumo au ilikuwa changa la macho?
 
Kuna jambo halieleweki hapa, watu wanatoa sababu hazina mashiko.

Hizi namba za simu zote zimesajiliwa tena kwa ganda la taifa ikiunganisha majina yako na unapoishi na kama namba ni ya mtu mwingine hauwezi kusajiliwa.

Leo eti mfumo mpya kwa majina yako, means hii techn ya sasa ni fake!.
Italeta shida labda watupe tuone inavyofanya kazi
 
tatizo la mtanzania .ukiwekewa mfumo utaorahisisha huduma na pia usikoser kutuma tayar unaanza kuweka assumptions zako za kijinga.unaambiwa hapo gharama itashuka bado unakua na mawazo mgando.kwan aliyekwambia walikua hawapat sent hata katika hii mufumo ya awali nan?
Tuliza kipapa binti!! Usijilazimishie kwangu bit----ch
 
Msipokuwa makini mtaibiwa....badala kumtumia gaudensia G mapunda, linakuja jina gaudensia B mapunda....ona sasa
 
Tangu gavana aseme kuwa watoa huduma za fedha kwa njia ya simu kusajiliwa nchi nzima kutasaidia kuzipunguza gharama za utumiaji na utoaji wa fedha sijaona mabadiliko yyt zaidi ya gharama izo kupanda mara dufu.
Hii mitandao ya simu inatupiga hela nyingi kuliko kawaida kupitia gharama za utoaji na utumaji
 
Hua najaribu kutafakari kwakweli, ni kwamba hivi wananchi sisi tukikazana kutafuta pesa kwa ajili ya familia zetu wanaona kua tunafaidi sana..nchi hii mwananchi akiwa na pesa au watanzania wakifanikiwa maisha sio sawa ,
Ukiwa na pesa usipokuwa maskini unaye struggle wewe siyo mzalendo, huku wao wanatembea na maviete!

Everyday is Saturday................................šŸ˜Ž
 
Dar es Salaam. Kuanzia Julai Watanzania wataweza kutuma fedha haraka kwa watu waliopo kwenye orodha zao za mawasiliano ya simu bila kutafuta namba za majina husika.

Hiyo itawezekana kwa sababu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itazindua mfumo wake wa Malipo ya Haraka (Tips).

Tips itahamasisha miunganisho ya huduma za fedha za kidigitali yakiwamo malipo kwa watoa huduma kwa gharama nafuu na zenye ulinzi.

Mfumo huo utafanya kazi kwa njia ambayo malipo yote ya kidigitali, yakiwamo ya miamala ya simu kama Airtel Money, Tigo Pesa, M-Pesa, HaloPesa, EzyPesa na T-Pesa, itakayounganishwa katika jukwaa moja.

Kwa hiyo, mtu anayetaka kutuma fedha atahitajika kuwa na jina la mtu anayetaka kutumiwa kabla ya kutuma.

Mfumo huo unaelezwa utarahisisha utumaji wa fedha na kupunguza gharama.

Awali, mfumo huo ulitarajiwa kuanza kufanya kazi Desemba mwaka jana, lakini Mkurugenzi mifumo ya malipo wa BoT, Bernard Dadi alisema waliamua kuuboresha kwa kuubadilisha na kuujenga upya.

ā€œMpango huo unatarajiwa kuwa tayari katika awamu ya kwanza Julai mwaka huu,ā€ alisema Dadi.

Awamu hiyo itahusu biashara ya mtu kwa mtu.

Dadi alisema baada ya awamu hiyo ya kwanza, kutakuwa na awamu ya pili, ya tatu na mwisho awamu ya nne itakayohusisha ulipaji wa kodi na malipo ya jumla na mengineyo yatakayojitokeza katika masoko.

Pia, alisema, utekelezaji wake pia ulipangwa kuanza Juni, mwaka jana lakini kutokana na maambukizi ya virusi vya corona ulihifadhiwa kwanza.

BoT iliisitisha timu liyokuwa ikitekeleza mradi huo kutokana na maambukizi ya corona na kuanzisha timu nyingine.

Hata hivyo, baada ya kuundwa kwa timu nyingine mfumo huo haukuweza kuzinduliwa kwa muda uliotarajiwa yaani Juni na ulisogezwa hadi mwisho wa mwaka jana.

Maandalizi ya matumizi ya mfumo huo ambayo yatafanyakazi kupitia kadi za malipo, benki za simu, uchumi wa kidijitali na benki za intaneti, yalianza kufanyika tangu Juni 2018. Na matumizi hayo yalipangwa kufanyika kwa bidhaa za fedha na kwa watoa huduma.

Matumizi ya mfumo huo yanalenga kupunguza matumizi ya fedha tasilimu katika malipo na katika uchumi.

CHANZO: Mwananchi
Sawa tumewaelewa
 
M bona

Mbona Airtel hiyo huduma wanayo kitambo? Option ya mwisho ukishamtumia hela wanakuuliza Kama unataka kusave number ya uliyemtumia na jina lake ili next time usipate shida. Labda kama itakuwa na maboresho zaidi kama alivyosema mkurugenzi wa mifumo BoT
 
Naona nimekuwa mgumu kuelewa, najiuliza
1.Utapunguza vipi gharama?? Au mitandao ya simu itashinikizwa kupunguza makato?
2. Kwa sisi wenye namba nyingi, kutakuwa na options za kuchagua mtandao? Kama kutakuwa na options sijaona urahisi wowote..

Mwisho naona tutaanza kufatiliwa transactions zetu sasa....kwa wale tunaofanya malipo na kuuza kwa njia ya simu...Tunaweza kuongezewa kodi wakiona transactions ni nyingi..
Nadhani hiyo ndio target yao. Hakuna maboresho yoyote, makato no yaleyale tu
 
Back
Top Bottom