Adqcos
New Member
- Jul 20, 2022
- 2
- 0
Ijapokuwa changamoto za mfumo huu huwa zipo maeneo mbalimbali lakini napenda kujikita zaidi kwa wahitimu wa kada za Afya nchini ambao ni Madaktari, Afisa Tabibu, Wauguzi, wateknolojia Dawa, Wateknolojia Maabara na Afisa Tabibu Meno.
Mifumo ya elimu kwa ajili ya kumuandaa mtu wa kusomea taaluma zilizotajwa hapo juu ni mara nyingi huwa inawabana wataalamu hawa kujihusisha na masomo mengine kama vile ya tahasusi za kiuchumi na sanaa lakini baada ya muhitimu kumaliza masomo yake hushauriwa kuweza kujiajiri ijapokuwa hakupewa elimu itakayomuwezesha kufikia malengo ya kujiajili kama ushauri wa kumtaka ajiajili usemavyo.
Elimu yetu ya sekondari ndio msingi wa taaluma zetu tangu ukiwa sekondari mtu unajiandaa kuwa mtu fulani au na taaluma fulani kwa kupokea ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wa karibu ili kuwa mtu fulani au na taaluma fulani basi huna budi kujikita zaidi kwenye masomo ya tahasusi za sayansi hii inamuandaa moja kwa moja aje kuwa na taaluma izo za afya.
Siku akifanikiwa kuhitimu masomo ya tahasusi za Sayansi atakapofanikiwa kujiunga na elimu ya chuo anaanza kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na masomo hayo anayasoma kwa muhula mmoja pekee na kumtaka mtu huyu baada ya kuhitimu ajiajiri. Lakini pia tunapaswa kutambua kuwa kuna wanafunzi ambao walijikita zaidi na tahasusi za biashara na wengi wao baada ya kuhitimu wanasema wako tayari kujiajiri kuliko kuajiliwa.
Hii inatokana na mifumo ambayo iliwaandaa tangu wakiwa sekondari mpaka anapohitimu masomo yake ya elimu ya juu. Hivyo kitu icho huwafanya wataalamu wengi wa afya kuwa tegemezi wa ajira na sio watu wa kujiajili kwakuwa amekwishakuandaliwa kwa ajili ya kuajiriwa tu.
CHANGAMOTO YA AJIRA
Pamoja na watu hawa kuandaliwa kuwa tegemezi zaidi kwenye kuajiliwa kwa kipindi hiki kumekuwa na changamoto ya ajira kwa wahitimu wa mafunzo haya ya kada izo za Afya. Mfumo umebadilika tofauti na ilivyokuwa hapo awali mfumo wa ajira ulikuwa ni rafiki kwa wahitimu wa kada hizo za afya ilikuwa mara baada tu ya kuhitimu mafunzo hayo kulikuwa na asilimia 100% za kupata ajira serikalini na ikiwa kuna aliyechelewa kupata nafasi hiyo ya ajira ilikuwa haizidi miezi 6 watu wote wasiokuwa na ajira wanakuwa wameajiriwa tayari.
Kutokana na changamoto iyo ya ajira kutopatikana kwa uhakika serikalini wahitimu wamekuwa wakiajiriwa katika taasisi za afya za binafsi taasisi ambazo zinatumia nafasi ya ukosefu wa ajira za kudumu serikalini kama fursa ya kujiingizia kipato huku zikitumia rasilimali watu kwa kutowalipa viwango vya mishahara ya kuridhisha yaani kwa dhuluma au kuwanyonya watu hawa.
Na wakati huo wakiamini ya kuwa hauwezi kuacha kazi kwakuwa wewe ukiacha mwenzako atakuja kuifanya kazi iyo yamkini hata kwa kiwango cha chini cha mshahara kuliko kile unachotaka kulipwa wewe au unachokikataa kwakuwa wapo wahitimu wengi mtaani wasio na ajira. Mfano wake ni Zahanati, Maduka ya dawa muhimu, Maabara binafsi, Vituo vya Afya na Hospitali.
MADHARA YATOKANAYO NA UNYONYAJI HUU
Baada ya wahitimu wengi kumaliza mafunzo ya fani zao huwa na tegemeo la kuzisaidia familia zao mara baada ya kumaliza mafunzo yao. Hii inaweza kuwa kwa kujua au kutokujua watu hawa wanaomiliki taasisi hizo za binafsi hawamuathiri mtu yule tu waliyemuajiri kwenye taasisi zao lakini pia wanaathiri na familia zao kwakuwa watu wengi wanajitahidi kusoma huwa wanatokea kwenye familia zenye uchumi duni kama sio wa chini kabisa hivyo wakati mwingine familia huwa zinajinyima kwa kujitoa muhanga ili mmoja wa wanafamilia aweze kusoma na wakiamini baada ya kufanikiwa kwake atakuja kuwasaidia.
Lakini kutokana na unyonyaji unaotekelezwa na hawa wamiliki wa taasisi hizi za binafsi hapa nchini Tanzania watu hawa walioaminiwa na familia kuja kuwa wakombozi kushindwa kutekeleza ahadi ya kusaidia familia zao kwa kutopata kipato rafiki kinachoendana na gharama za maisha ya sasa ambazo kiuhalisia ni kujikimu binafsi lakini pia kushindwa kugawanya kipato icho mara mbili kwa maana ya kuisaidia na familia yake na wategemezi wake.
Pia kitendo icho husababishia serikali kukosa mapato kwa maana wafanyakazi hawa huwa hawana mikaba ya kudumu hivyo wanakosa hisani ya kusajiliwa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii na mfanyakazi pia halipi kodi.
Vilevile kitendo hicho husabibisha wadau wa afya kupungua kwa taasisi za binafsi na kupelekea watumishi wa afya kwenye taasisi za binafsi kukosa mafunzo kwakuwa wanakuwa sio wafanyakazi wa kudumu na niwenye kuhama hama sababu wanaondoka kwenda kutafuta taasisi ambayo inakuwa walahu inamaslahi ya juu kidogo na kusababisha wadau wa afya kushindwa kufuatilia utekelezaji wa mafunzo waliyoyatoa.
NINI KIFANYIKE
Kutokana na changamoto hizo nilizoziainisha hupelekea wahitimu hawa wa fani hizo za Afya uona kuajiriwa serikalini ni salama zaidi kuliko kwenye taasisi za binafsi na kuona wimbi la vijana wenye uhaba wa ajira limekuwa kubwa zaidi.
Watu wanaopatiwa dhamana ya kusimamia sheria za kazi wawe wazalendo kwakuwa wanapokuja kukaguwa wanapokuta mapungufu wasimamie sheria na sio kupokea rushwa.
Kuwe na viwango maalumu vya mishahara kwa taasisi za binafsi kama ilivyo serikalini, hii itasaidia kupunguza wimbi la vijana wenye uhaba wa ajira na kumfanya afurahie kazi.
Sheria ya kuwaunganisha wafanyakazi wote wa taasisi binafsi kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii itafutiwe mbinu mpya ya utekelezaji ili kuondoa dhuluma inayoendelea.
Itungwe sheria yenye utekelezaji na usimamizi makini wa kuwaunganisha wafanyakazi wote wa taasisi za binafsi kwenye vyama vya wafanyakazi.
Awepo muwakilishi wa taasisi binafsi kwa kila ngazi ya utawala kwa sekta ya afya kama ilivyo kwa sekta za afya za serikali na atambulike kisheria, hii itasaidia hata kupunguza rushwa wakati wawakilishi wa mamlaka yenye dhamana wanapokuja kufanya ukaguzi na muwakilishi wa taasisi binafsi akiwepo.
Hii pia itasaidia kupunguza changamoto ya ajira inayowakabili vijana wengi waliyohitimu mafunzo yao ya elimu ya vyuo vikuu na vyuo vya kati.
Ajira za taasisi za binafsi ziwe na usawa wa haki za wafanyakazi kama ilivyo kwa ajira za serikali na hii itawezekana iwapo sheria zinazotungwa kulinda haki za wafanyakazi zinapata wasimamizi wenye uzalendo na nia thabiti ya usimamizi na utekelezaji wake na ukiukwaji wake uwe na adhabu kali.

Upvote
0