Mfumo wa kuajiri kupitia Ajira Portal na kuita watu kwenye usaili physically mikoa ya mbali unamaliza pesa za serikali na wananchi

Ni matumaini yangu wote wazima. Mimi ni kijana wa kiume nimesoma diploma ya procurement and logistic management na bachelor degree ya business management, natafuta ajira nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote
Umemaliza mwaka gani?
 
Cheating itakuwaje kubwa ukiwa na dedicated stations? Weka station Duce, UDSM, IFM, Uhasibu ama wawe na vituo vyao maalum kabisa vya kikanda. Sio lazima wote tukarundikane Dodoma.

Najua viongozi wenye kampuni za mabasi hawawezi kubali hio ishu iondolewe maana huwa wanapiga hela.
 
Ngoja tuone
 
Hatuna Internet ya Uhakika maeneo yote Nchini.

Imagine kuna baadhi ya maeneo hapa Mkoani Dar, Internet inasuasua.

Je, kule Vijijini hali ikoje?
Hiyo sio excuses ukitaka Kufanya interview tafuta eneo lenye interview.

Mbona vyuo watu wanaomba online nchi nzima
 
Sekretariet ya ajira ni mojawapo ya taasisi inayotakiwa kufutwa ni matumizi mabaya ya kodi ya wananchi na kusumbua wananchi hakuna value yoyote wanayoi-add zaidi ya mfumo wa upendeleo na rushwa. Waomabji waombe direct kwa mwajiri kama zamani.
 
Kuna interview nilifanya Ile KAZI ilikuwa Uingereza.

Kuna link walinipa ilikuwa ni video interview.

Ukifungua Ile link unakuta swali halafu unabonyeza Hilo swali camera ya simu au laptop inafunguka inakubidi uanze Kujibu. Unapewa dakika 1 au 2 Kujibu. Hizo dakika zikiisha video inajifunga yenyewe. Linaingia swali la pili Hadi umalize maswali yote.

NB: Hiyo video interview hupaswi kuangalia pembeni na wala unakuwa huulizwi maswali na MTU maswali yanakuwa yamewekwa kwenye text. Na ili ujue swali linalofuata lazima umalize na submit video uliyojirecord ya swali la Kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…