KERO Mfumo wa uhamisho kwa watumishi mwaka 2023 umekuwa kero kubwa

KERO Mfumo wa uhamisho kwa watumishi mwaka 2023 umekuwa kero kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa uhamisho kwa watumishi mwaka jana 2023 watumishi wamekuwa na kilio kisicho na mtu wa kunyamazisha, kwa maana hakuna mtumishi aliyeomba uhamisho na akapata kibali cha kuhama kwenye mfumo.

Mbaya zaidi ukipiga simu TAMISEMI hata wao hawajui ni lini vibali hivyo vitatoka, kiukweli watumishi wenye uhitaji wa kuhama wanapitia tatizo kubwa kisaikolojia maana wanazo sababu za kuhama ila hawaoni dira katika hilo. Wapo kazini kimwili ila mawazo yao yote yanawaza uhamisho.

Tunaomba Katibu Mkuu alifanyie kazi suala hili.

Soma Pia: Mfumo wa Mtandao kuomba uhamisho Serikalini ni tatizo, unatakiwa kuboreshwa
 
Andika barua, watu mwaka huu wameandika barua na wamepata vibali kupitia barua walizoandika.Ukisubiri uhamisho wa mfumo hutahama.
 
Mmh,ila watu wanahama,kuna kitu imenichekesha sana,barua zilisainiwa desemba mwaka jana,zimekuja kufika halmashauri mwezi septemba.
Cha kuchekesha bado kuna halmashauri bado zinaficha hizo barua.
Kufanya kazi chini ya tamisemi ni laana
 
Tamisemi mmenilamba block haya njoo mtambie kwa nini vibali vya tangu desemba vinafika sasa hivi?je mmetoa agizo kwa halmashauri wawape watu vibali vyao?hamjui kama wanavificha?
 
Back
Top Bottom