Mfungwa aliyepatiwa msamaha wa Rais agoma kutoka jela

Mfungwa aliyepatiwa msamaha wa Rais agoma kutoka jela

Katika hali ya kushangaza Merad Abraham ambaye ni miongoni mwa wafungwa 70 waliosamehewa na Rais John Magufuli jana Disemba 9, amekataa kuondoka katika gereza la Ruanda mkoani Mbeya akidai kuwa hana mahala pa kwenda huku akijijeruhi usoni kwa jiwe kwa nia ya kutaka arejeshwe katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Meradi ambaye alifungwa kwa kesi ya kubaka alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Juni 20, 2000 na alitakiwa kumaliza kifungo Juni 20, mwakani.

Kwa sasa mfungwa huyo amepelekwa kwenye zahanati ya gerezani kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

#AzamUTV #AzamTVTZ #AzamTWO #AzamNewsView attachment 1287707View attachment 1287708
Mbona usoni usoni damu zinamtoka? Maaskari wamemfanya nini?
 
Watu walitabiri haya kutokea - hongera Magufuli kwa kutufungua macho tunajifunza kuwa si wote wanapenda kuishi uraiani

Safari hii wafungwa wamechukia na kununa kwa kupewa msamaha tofauti na zamani waliosamehewa walikuwa wanatoka na furaha mpaka wanatoa machozi ya furaha
 
Safari hii wafungwa wamechukia na kununa kwa kupewa msamaha tofauti na zamani waliosamehewa walikuwa wanatoka na furaha mpaka wanatoa machozi ya furaha

Mtaani kupo dry bora kurudi jela kuna uhakika wa kula na kulala at 0 cost
 
Kuna magereza askari mwenyewe anakuwa kama mfungwa sembuse mfungwa mwenyewe atakuwa kwenye hali gani, kwa gereza la ruanda sina uhakika. Baadhi ya wafungwa wanapiga sana kazi tena zaidi ya watumwa pamoja na kupigwa fimbo na manyapara pale anapoonekana kuwa mkaidi. Kwa mfungwa wa keko na ukonga ndio anaweza sema yupo picnic. Nenda gereza la wazo au kigamboni kwa DSM tuu utaona mazingira ya wafungwa wanayoishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aache woga wa maisha zile kaz alizokua akifanya kwa kusimamiwa akazifanye kwa kujisimamia yy mwenyewe
 
Back
Top Bottom