Mfungwa aliyepatiwa msamaha wa Rais agoma kutoka jela

Mfungwa aliyepatiwa msamaha wa Rais agoma kutoka jela

Aisee, psychologically hayuko sawa, huenda anawaza akija mtaani ataanzia wapi Maskini, mwaka 2000 ndyo nilikua naanza std 1 now nishamaliza chuo mda mrefuu dah, ujana wote ndani[emoji30] [emoji30]
 
Kweli, hayuko sawa huyo
Huyu jamaa ndio yuko sawa kuliko hao wengine waliopewa msamaha..

Kutoka maisha ya Gerezani kwenda maisha ya Uraiani bila mataarisho sio rahisi.

Magereza yetu hayapo kwa kuwafundisha na kuwatayarisha wafungwa maisha baada ya kumalizana kifungo..

Sasa wewe unategemea jamaa atafanya nini Uraiani wakati yeye ameshajijenga kisaikologia kuwa maisha yake yatamaliIkia jela??
 
Daa! Wee jamaa umeua kila kitu.
Atakuwa amesimuliwa hali ya kitaa. Kaambiwa juu ya unga, kaambiwa juu ya ajira, kaambiwa juu ya upatikanaji wa pesa kaona achague fungu jema kwake.
 
Katika elimu ya utafiti na uandishi wa habari, kauli ya mtu mmoja kati ya 5,533 haikubaliwi.

Katika uandishi wa habari, kauli ya mtu (source) mmoja haiaminiki mpaka walau maneno yake yathibitishwe na watu watatu.

Katika taaluma ya Utafiti hali ndio ngumu zaidi kwani inatakiwa asilimia 20 (sample) ya watu wote (population) ndio tupate kugeneralize kitu.

Hivyo basi, wanaopayuka kwa sababu ya kauli ya mfungwa mmoja hawana hoja inayokubalika kisomi bali ni dhihirisho la ujinga uliogubikwa na maslahi ya kisiasa.

Badala ya kutafuta njia ya kumsaidia matatizo ya kisaikolojia yanayomkabili kijana huyu, wao wanamgeuza *dili* la kujivunia umaarufu.

Hivi hawakuisikia ripoti ya benki ya Dunia inayosema umasikini umepungua nchini???
 
Hapo juzi mheshimiwa raisi John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za uhuru huko Mwanza aliwasamehe wafungwa takriban elfu tano unusu.Mwenyewe alisema amewasamehe wengi sana na kweli ni wengi.Alitaja vigezo vya kuaachiwa kwao na sababu zake.

Kitendo hiki cha huruma kutoka kwa maraisi hutendeka kila mwaka na sijui kwanini lazima iwe siku ya uhuru na isifanyike ikulu siku yoyote ile.Idadi hii kubwa ya wafungwa na mahabusu ni dalili ya kasoro na mapungufu ya vyombo vya kisheria ambapo hatimae huzaa uonevu mwingi unaopelekea mrundikano magerezani na mahabusu.

Linaloshangaza huruma hizi za raisi bado hazijawagusa wale masheikh wetu kwa nyakati zote kwa wale wanaotakiwa kukiri makosa wakatoka wala wale wanaosamehewa tu kama hapo juzi.Wengine wameseamehewa kwa kuwa makosa yao ni madogo na wapo waliofungwa kwa kuonewa tu.Hawa masheikh wangestahiki zaidi kusamehewa kwani makosa yao pamoja na muda kuwa mrefu wa kukaa magerezani bado makosa yao hayajajulikana.Ni sarakasi tu.
 
Samehe sabax70 mkuu,😄kashajihakikishia kura buku5 na ushee kwa 2020 GE..😂😂😂🚶🏿🚶🏿🚶🏿
 
Back
Top Bottom