Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Hata mi nawaza hili. Kumpa mtoto life skills za kusaka noti. Na zaidi sana napingana sana na usemi mtoto urithi wake elimu mi nimejipangia kupambana niwezavyo niwape mali...kabla sijafa sio aje arithi nikiwa mfu.

Kuna dogo mmoja ana urafiki na ndugu yangu...ndugu yangu alifeli kidato Cha nne zeroo...akajifunza udereva mitaani nikamtafutia leseni.... yuko anapiga zake kazi za udereva, ana maisha yake na mke na mtoto kukiwa na Jambo kwenye familia anachangia. Sasa huyu rafiki ake Ni msomi wa digrii ametoka zake huko mkoa anamsumbua ndugu yangu amtafutie ajira na anaishi kwake hana analofanya zaidi ya kusumbua kwa simu apate ajira. Ndugu yangu anahangaika sana....

Mfano wa pili huyu ndugu yangu ni age mate na mdogo angu wa kiume.....ye kasoma digrii na amesoma school of law hana ajira mpk Leo hi hopeless hana analofikiri zaidi ya kula bata tu...hakuna analoweza walikuwa wakimcheka huyu ndugu kuwa hana elimu...lkn ana maisha yake...anajitegemea..... Yaani huyu dogo anashindwa hata kufikiri kutumia taaluma yake ya sheria kujiajiri hana...anawaza tu kuajiriwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuwaje kama utatangulia wewe?
 
You are very right Madam, tatizo watu wengi hawana msingi wa elimu za biashara hata kama ni informal inasaidia sana kujua abcs za business.

Binafsi niliingia kwenye biashara baada ya kumaliza form 4, na hapo sijui ilitokeaje nikakosa post ya form 5 na nilikuwa na division 2 na kwa miaka hiyo ilikuwa ni pass mark nzuri sana.

Kutokana na changamoto za kifamilia sikuweza kuafford private school nikazama mtaani. Nikafanya business kwa miaka 4 then nikaenda advance baada ya hapo chuo nikaunga.

Nilipomaliza nami nikajikuta kwenye mtego wa wahitimu wa kusaka ajira wakat nilikuwa na balance nzuri tu baada ya kutoka chuo kwa kuwa muda wote nasoma nikiwa likizo nilikuwa napiga mishe zangu nasave pesa.

Baada ya kuapply kwa miezi kadhaa huku nikitumbua 'mafao' yangu, nikatafakari hapa nisipojiongeza nitaishiwa. Nikaamua kuset deadline ya kutafuta ajira (mwaka mmoja tu) ndio muda niliojipa tangu nitoke chuo. Ulivopita sikuapply tena na hata ndugu na jamaa walipo nitonya kuna nafasi mahali niliitikia ila kiukweli sikuapply kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mhh tutaonekana tunawananga waloajiriwa...!mie siwez soma had Msc eti take home ikawa laki 6!
 
Hata mi nawaza hili. Kumpa mtoto life skills za kusaka noti. Na zaidi sana napingana sana na usemi mtoto urithi wake elimu mi nimejipangia kupambana niwezavyo niwape mali...kabla sijafa sio aje arithi nikiwa mfu.

Kuna dogo mmoja ana urafiki na ndugu yangu...ndugu yangu alifeli kidato Cha nne zeroo...akajifunza udereva mitaani nikamtafutia leseni.... yuko anapiga zake kazi za udereva, ana maisha yake na mke na mtoto kukiwa na Jambo kwenye familia anachangia. Sasa huyu rafiki ake Ni msomi wa digrii ametoka zake huko mkoa anamsumbua ndugu yangu amtafutie ajira na anaishi kwake hana analofanya zaidi ya kusumbua kwa simu apate ajira. Ndugu yangu anahangaika sana....

Mfano wa pili huyu ndugu yangu ni age mate na mdogo angu wa kiume.....ye kasoma digrii na amesoma school of law hana ajira mpk Leo hi hopeless hana analofikiri zaidi ya kula bata tu...hakuna analoweza walikuwa wakimcheka huyu ndugu kuwa hana elimu...lkn ana maisha yake...anajitegemea..... Yaani huyu dogo anashindwa hata kufikiri kutumia taaluma yake ya sheria kujiajiri hana...anawaza tu kuajiriwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni muhimu sana yani kuwajenga watoto kukabiliana na maisha toka utotoni. Yani mtoto ajue kuisaka sh.100 yake hata ikibidi before hajaanza sekondari awe amejifunza life skills za kumuingizia pesa bila kutegemea mtaji zaidi. Akishafika form 4 ndo unamu introduce kwenye mtaji.
Watu tuliowadharau hawana elimu leo hii ndio waliopiga hatua zaidi kimaisha kuliko tunaojiita wasomi. Usomi bila pesa na kujimudu kimaisha its nothing.
 
Yani kwa Tanzania ya sasa uanze kuuza nyanya uwe milionea thubutu semeni tu waajiriwa wasikae kizembe wafanye chochote wapate hata hela ya bando ila kwa bongo hii ya 2020 utoke from zero uwe milionea sahau....

Sent using Jamii Forums mobile app
Bongo kupiga hela awamu hii ni lazima uwe una pesa ya maana kwenye mzunguko. Unaokota buku mpaka buku 5 huku na kule ndio hapo unajikuta umezivuta nyingi.

Ila kwa mtaji wa Laki 5 kwa faida za 50-100 utakunywa sana Spar-letta Bar. Unajikuta umemeki 12,000 siku nzima ukijimix unatafuna mtaji.
 
Pesa ya maana inaanzia kiasi gani?
 
Ha ha punguza hasira mkuu..
Acheni kutudanganya vijana ooh sijui mkajiajiri sijui ajira hazina hela pumbavu zenu mbona nyie mmekomaa hukohuko maofisini kwenu tunawaona mnagenga magorofa na kununua magari ya kifahari alafu mnakuja humu mnasndika upumbavu sijui mtu mwenye degree akauze nyanya mamaee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo kupiga hela awamu hii ni lazima uwe una pesa ya maana kwenye mzunguko. Unaokota buku mpaka buku 5 huku na kule ndio hapo unajikuta umezivuta nyingi.

Ila kwa mtaji wa Laki 5 kwa faida za 50-100 utakunywa sana Spar-letta Bar. Unajikuta umemeki 12,000 siku nzima ukijimix unatafuna mtaji.

Mkuu 12000 kwa siku ni hela nzuri sana tumia 4000 tunza 8000 ukiidharau hiyo hata 3m utaidharau
 
Tanzania haina competition kwenye biashara nyingi, vitu ambavyo vimefanywa nje havijafanywa Tanzania ni vingi mno, alafu vijana wengi wamelala wanategemea ajira kwa hiyo ukianzisha kitu kipya wao watakaa kuendelea kukaa ofisini wanakuoa tu unapiga hela. Nipo nje miaka mingi sasa na trust me huku kuanzisha kitu kipya ni ngumu mno karibia kila kitu washafikiria wengine wakafanya, na ukipata kitu kipya kama kina potential wapo viijana wengi smart na wana hela watajaribu kushindana na wewe wakule kichwa kabla hata hujatoka. Tanzania unaanzisha kitu kila mtu amelala wanakuangalia tu.
Ni vema kwa vijana kujifunza na kuwapa motisha zaidi unatolea na mifano wa ivyo vitu ili kama walikuwa hawajakifikiria basi unakuwa umewasidia na siyo kusema idea huko zipo ila huku hakuna na huzitolei mifano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikujaga dada mmoja humu JF kipindi cha nyuma,Full kujiita ladyboss,ponda sana vijana waliomaliza chuo akisema wapambane wasitegemee ajira tu,full kushauri vijana wapambane sana la sivyo atawalea mwenyewe kwa pesa zake mara paaaap ID ikaunganishwa na ID yake nyingine akitafuta mteja wa kununua kitanda chake na godoro lake used maisha yamekua magumu anataka kusepa mjini,hahah

Nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiii,modes ni Konyo sana aiseeeee.
Wanatumia njia gani kujua hizi Ids ni za mtu mmoja ?
 
Mnataka nitaje mi CEO wa kampuni flani ili muanze kunitafuta? JF watu anonymous siwezi jitaja hapa umeona barua wanazotumiwa jf kuomba habari za users?
Nitakucheki kwa Id yangu nyingine ili tuyajenge mkuu
 
Ni vema kwa vijana kujifunza na kuwapa motisha zaidi unatolea na mifano wa ivyo vitu ili kama walikuwa hawajakifikiria basi unakuwa umewasidia na siyo kusema idea huko zipo ila huku hakuna na huzitolei mifano

Sent using Jamii Forums mobile app

Haha napata point yako ila sio entrepreneurship hiyo, wanasema mfundishe mtu kuvua samaki sio kumpa samaki, kama wanataka ideas kuna thread moja humu mtua alipost idea zaidi ya 10 ambazo nyingi ukifanyia kazi unatengeneza mamilioni, in short kuna idea moja alitaja ambayo hata mimi nilikua nshaanza kuifanyia kazi.

Kua entrepreneur mzuri solution ni moja tu, angalia tatizo ambalo lipo kwenye mazingira yako, tafuta solution yake na solution iwe ambayo watu wanaweza kulipia, alafu solve hilo tatizo watu wakupe hela. Kila biashara ndivyo ilivyo.

Sasa bongo matatizo mbona yamejaa mno? Na kama mtu hana capital akianza kuimplement idea hata kwa hela kidogo anaweza fika sehemu akaomba investment makampuni yapo mengi yanatafuta watu wanaojaribu kitu kipya wainvest, hata mimi mwenyewe ukija na kitu kipya na kinaweza tengeneza hela kweli umeanza kuexecute vizuri investment naweza toa mapema kabisa, just don’t come with an idea, njoo ukiwa umeishaanza kuexecute, napenda sana execution kuliko maneno tu.

Na nishapata jengo kubwa soon nitafungua incubator Dar es salaam ya technology kuleta startup companies mbalimbali bongo nawapa ofisi bure kabisa wakae waimplement wanachotaka, nawapa na msaada wa marketing kwenye sns, mabango ya barabarani ikihitajika au technical experties maana nina miaka zaidi ya 10 kwenye utengenezaji wa software.

Naomba vijana wa kitanzania muamke, acheni lawama, acheni excuses, hakuna mtu atakaa awasikilize, amka anza kupiga kazi, huna direction kaa uliza watu, kaa tafuta connection, tafuta like minded people, kila mtu ana strength zake na weakness zake, tafuta mtu opposite na wewe anayeweza kukupa nguvu aple ambapo una mapungufu, entrepreneurship una challenge zake kibao ila trust me ukihit ni biashara moja tu unachomoka kabisa unasahau umasikini.
 
Huyo unaweza mshauri ajiingize kwenye kujiajiri lakini, japo asiache kazi yake moja kwa moja ila hata akimiliki duka lenye groceries sio mbaya.
Unamshauri nini mwalimu wa degree maana hata hiyo ajira akiipata Take-home unaweza kuta 600K.
 
Graph, Ni kweli kaka ila business idea huweza pia kupatikana kwa kujifunza kutoka kwa mtu ulio ona anafanya kwa iyo itakuwa siyo mbaya hizo idea za wengine ukazitoa ili tujifunze pia

Tupe hizo idea angalau tupate kitu cha kuanzia. idea ambazo hazitahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia ili hiyo dhana ya kuachana na kuajiriwa iweze kuondoka kwenye mind zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Twende practical... Mfano uyo jamaa wa law anahitaji kujiajiri ila iyo biashara unahitaji 100K na iyo K hana, unasemaje anawaza kuajiriwa tu.
Hata mi nawaza hili. Kumpa mtoto life skills za kusaka noti. Na zaidi sana napingana sana na usemi mtoto urithi wake elimu mi nimejipangia kupambana niwezavyo niwape mali...kabla sijafa sio aje arithi nikiwa mfu.

Kuna dogo mmoja ana urafiki na ndugu yangu...ndugu yangu alifeli kidato Cha nne zeroo...akajifunza udereva mitaani nikamtafutia leseni.... yuko anapiga zake kazi za udereva, ana maisha yake na mke na mtoto kukiwa na Jambo kwenye familia anachangia. Sasa huyu rafiki ake Ni msomi wa digrii ametoka zake huko mkoa anamsumbua ndugu yangu amtafutie ajira na anaishi kwake hana analofanya zaidi ya kusumbua kwa simu apate ajira. Ndugu yangu anahangaika sana....

Mfano wa pili huyu ndugu yangu ni age mate na mdogo angu wa kiume.....ye kasoma digrii na amesoma school of law hana ajira mpk Leo hi hopeless hana analofikiri zaidi ya kula bata tu...hakuna analoweza walikuwa wakimcheka huyu ndugu kuwa hana elimu...lkn ana maisha yake...anajitegemea..... Yaani huyu dogo anashindwa hata kufikiri kutumia taaluma yake ya sheria kujiajiri hana...anawaza tu kuajiriwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio muanze nyie kuonyesha mifano ya hawa mnayoandika humu. Anzeni nyie kujiajiri ili watoto wenu waige waone kumbe inawezekana.
Wengi wenu wenye ajira hamjawahi ata kufungua banda la kuonesha mpira ila ndo mko mstari wa mbele vijana wajiajiri vijana wajiajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikwel hawakuwah kufungua biashara kwasababu wamebahatika/wamefanikiwa kupata ajira,ila pale walipo makazin wanakutana na changamoto ambazo wao wanawahimiza ninyi msiyo ajiriwa mzichangamkie(kwani vibaya kuambiwa haya??)
Hata hivyo nikutoe tongotongo, waajiriwa wengi ndo wanaongoza kwa kutoa mitaj midogo na ya kati kuwawezesha wasiyo na ajira, siyo lazima wao wafanye
ila mimi mwenyewe nshasema huko juu nimeajiriwa na kuna kazi 2 za ziada nafanya.1 yangu mwenyewe nyingine nipo chini ya mtu!!

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
 
Uhalisia 100[emoji2398] tazama jamii zinazokuzunguka.

Mtoto wa mfanya biasha
ra hata akisomea udaktari eventually elimu yake ataielekeza kwenye biashara zaidi.

Huwezi mfundisha mtoto kwa maneno matupu. Mtoto huiga kiurahisi zaidi.

Huyo anaetoka veta akitokea ukoo wa wafanya biashara kuna uwezekano mkubwa akaja kuwaajiri wenzake aliokuwa nao veta wanaotokea ukoo wa waajiriwa.

Mleta mada poyoyo na bado hajayaona maisha kiuhalisia wake.
We mama acha kutukana watu hovyo

One love
 
Back
Top Bottom