Mgahawa maarufu hapo Tabora maarufu kwa 'chotara" wahudumu awajali wateja

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
6,788
Reaction score
16,227
Katika majukumu yangu ya kila siku leo nilipita Tabora mjini nikielekea mpanda Katavi katika hali ya kupata chochote kitu ikanibidi niulizie mgahawa ambao ninaweza kupata chakula kizuri, kulingana na uchumi wangu.

Wenyeji wakanielekeza eneo lile Kuna mgahawa Al maarufu kwa "chotara" kwa nje ya mgahawa ule Kuna vijana wanaouza vitafunwa kama maandazi, chapati na sambusa, nikachukua chapati zangu tatu kwa vijana wale na nikaingia ndani ya mgahawa, nikatafuta meza yangu nikaketi ili nisubiri huduma nyingine kutoka kwa wahudumu, mgahawa huu umesheheni wahudumu wa kike wanaovaa ushungi..

Kitu Cha ajabu niliwaita wahudumu zaidi ya mara tatu lakini wote walikuwa wakiniangalia kama sanamu la posta😁. Muda uleule niliokuwa nimekaa akaja jamaa mwingine nae akaita wahudumu zaidi mara tatu lakini wahudumu hawakutokea hata mmoja.

Shime kama Kuna wamiliki wapo humu nawapeni taarifa kuwa wahudumu wanawaharibia biashara na wanawafukuzia wateja nimeambatanisha na picha za eneo hilo..
 

Attachments

  • IMG_20250321_200158.jpg
    370.7 KB · Views: 48
Tafuta hela mkuu. Huenda walikuona tangu stendi ukiwa unashuka kwenye basi huku unakula miwa.
 
Unakulaje sehemu chafu kama hiyo?
 
Au hawapati mshahara,au Salumu Kali?!!Hata kama mteja ni mfalme wanaharibu!
 
Itaku mtu wa kigoma

Hata hili ni la kuja kulalama JF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…