A
Anonymous
Guest
Mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro ila mkazi wa Tabata – Kimanga, Dar es Salaa. Kwanza ya yote nawashukuruni sana sana JamiiForums kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa kutusaidia kutatua kero mbalimbali zilizopo hapa nchini kwetu Tanzania.
Mimi kero yangu ni Sungusungu / Police jamii wanaolinda usiku, ndugu zangu hapa Tabata Kimanga, Mtaa wa Mbuyuni au maarufu kama Mtaa wa Majuva, tumekuwa na kero kubwa sana ya kusumbuliwa na Mgambo usiku.
Mgambo wanapita na marungu wanagonga kuta za nyumba usiku na wanapiga torch ndani ya nyumba / vyumba vya watu.
Nilishawashtaki kwa viongozi wa mtaa lakini bado ile tabia ipo. Ukiwauliza wanakwambia eti lazima tuwamulike ndani ili mjue tunalinda hatulali pia tunagonga ukuta mjue tupo.
Sasa hii imekuwa ni kero mno, mara nyingi usiku huo ni saa saba nane au tisa unakuta ndo Watoto wamelala, wakipiga ukuta au makelele yao wanaamka hata shule wanachelewa, sisi wenyewe akili inakuwa haifanyi kazi vizuri.
Ukiwaza usiku mara nyingi watu wanalala bila nguo sababu ya joto, wao wakipita wana torch kali mno wanamulika ndani. Pia, mapazia yanakuwa wazi kuruhusu hewa / upepo ndani.
Kiukweli wamekuwa kero kero kero sana sana. Mimi naamini ulinzi haupo hivyo hata wakati mmoja, wakipita ni wanapiga makelele mno mara wacheze na mbwa wao, mara wakae ukutani kwako waanze kuongea na simu wengine unakuta wanatongoza hata wanawake wao usiku kwenye simu.