Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,903
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Dr.Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo na kufuatiliwa kila mara na vyombo vya dola, kasema ni heri afanye shughuli zake binafsi kwa uhuru kuliko hivi ilivyokuwa.
 
TETESI: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo
Wataalamu wote wakiwa na misimamo ya kusimamia taaluma zao na sio kufanya kazi kwa matakwa ya wanasiasa ambao wengi wao hawaana utaaalamu hata chembe wa maeneo wanayo yaongoza, basi nchi yetu itafika mbali sana.
 
Kwani wakija na mambo yako vizuri tatizo linakuwa wapi,

Amesema mashinikizo, siyo kukaguliwa!.

Dr. Anashinikizwa kufanya kazi kama watakavyo wasio kuwa na taaluma. Taaluma inathamani sana.

Engineer, anashinikizwa kujenga miundo mbinu duni ili mradi finishing ing'ae. Muungwana ataona dhamira yake inamshitaki kwa madhara yatakayotokana na kazi yake, na hivyo akiona shinikizo hlio lisiol utaalamu linaendelea, ataachia ngazi. Huo ndio utamaduni tunataka. Lakini isje kuwa yeye ndiye anafanya kazi chini ya kiwango na anataka kuhalalisha kwa sababu zake binafsi. Huyo tutamwambia aende tu.

Hakimu binadamu, vile vile hatakubali kulazimishwa kupindisha hukumu kinyume cha sheria kwa kuwafurahisha watu wasio wana taaluma. Tuliona wa Nkurunzinza, aliondoka usiku kwa usiku na kuenda ukimbizini, akikimbia dhambi ya kupindisha sheria ili zimfae mtawala.

Huo ndio uungwana wa kitaaluma.

Dr. Ahsante kama umeilinda taaluma kwa ustawi wa Afya zetu. Kama umejiuzulu kwa sababu unataka kutetea na kuhalaisha uzembe, uende salama.
 
Wataalamu wote wakiwa na misimamo ya kusimamia taaluma zao na sio kufanya kazi kwa matakwa ya wanasiasa ambao wengi wao hawaana utaaalamu hata chembe wa maeneo wanayo yaongoza, basi nchi yetu itafika mbali sana.
Ni kweli mkuu. Tupo hapa tulipo kwa sababu ya siasa uchwara za wanasiasa uchwara.
 
Back
Top Bottom