Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Aende zake tu, nchi ina wataalamu wengi sana, wengine hawana ajira,

Sasa ana hofu gani kama kila kitu kinafanyika vizuri?
 
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Dr.Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo na kufuatiliwa kila mara na vyombo vya dola, kasema ni heri afanye shughuli zake binafsi kwa uhuru kuliko hivi ilivyokuwa.
Huwa inakera sana aisee, huyo kachelewa wengine tuliachaga enzi ya JK!! Nakumbuka kuna waziri nilimrushia makabrasha usoni nikasepa sikurudi tena hata baada ya kubembelezwa sana!

Hakuna kitu kinakera kama kilaz.a kukuingilia kwenye taaluma yako.
 
Na iwe kweli kwamba amechoshwa na mashinikizo,isije ikawa sakata la vyeti bandia tu.
 
Tuwe wazalendo.umesomeshwa na kodi zetu sisi tulioanza kazi miaka ya 80 halafu unakimbilia botswana? That is n't fair.
 
Bora aondoke,wasomi Kibao hawana kazi
Ajira moja hiyo ipo wazi.
Amana Hospital kwenyewe kila siku majanga tu,inaonekana amejitumbua mwenyewe.
Alizoea kufanyakazi kwa mazoea,na kama yupo above 45yrs basi ni muda wa kaachia,damu changa zichukue ajira.
 
Mganga mkuu kachoka yani kila kukicha mara kaja mkuu wa wilaya hajakaa vizuri kavamia waziri hajakaa vizuri mara kaja katibu, hajakaa vizuri kaja Makonda na makamera.
hii nchi kila mtu anajifanya anahusika na kila kitu.
Halafu bila mpangilio, wanaweza kugongana hospitalini wote. Sasa sijui dokta atamsikiliza nani at first
 
Bora aondoke,wasomi Kibao hawana kazi
Ajira moja hiyo ipo wazi.
Amana Hospital kwenyewe kila siku majanga tu,inaonekana amejitumbua mwenyewe.
Alizoea kufanyakazi kwa mazoea,na kama yupo above 45yrs basi ni muda wa kaachia,damu changa zichukue ajira.
Kumbuka unae msemea hapa ni daktari.... Taaluma inayo hitaji uvumilivu, uelewa na uzoefu wa hali ya juu... Daktari na wauguzi ni watu wa kuheshimiwa sana.. Taaluma sio ya kitoto
 
Big up daktari, ifike mahali wasomi wajielewe kama huyu. Utakuta kaKatibu tu wa afya au ka afisa utumishi kanamsumbua mtu na maelimu yake. IT HAS TO STOP. Wasomi wengine mjiongeze na nyie.
 
Nawaza tuu, unaweza kuletewa mtu kafa ukaambiwa useme bp
 
Back
Top Bottom