Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Huyu ana mapenzi mema kwa taifa lake na wananchi wake mana huwezi ingiliwa taaluma yako na kushinikizwa kufanya jambo fulani na mtu fulani kisa mkuu wa wilaya,au mkoa wakati hana anachokijua..kajitofautisha na wanaojiita maprofesa wa uchumi mtu anahojiwa kwanini pesa imeadimika na haipo kwenye mzunguko anakwambia na mimi naungana na kauli ya Rais kuwa kuna watu wanaficha pesa..kwanini usidhalilike kwa jamii
 
Huyu Dr mda si mrefu tutaskia kafariki kwa shinikizo la damu!! Alicho kifanya asingeogea angekaa kimya
 
Kama siasa imefika mpaka Mahospitali hii sio sawa na ni hatari sana.
Tuache unafiki madaktari na manesi Huduma zao Ni mbovu hivyo usimamizi WA Katibu unahitajika. Kama yy hapati guess ya kupiga deal asilete visingizio
 
Dokta hakupata ushauri mzuri kabla ya kufanya uamuzi huo.
 
Boooooraaaa congrats dokta shimwela....kisa cha kukosa amani ni nini....kapige zako private upate hela kwa raha zako .pesa yenyewe ndg maneno maneno mengi..
 
Big up daktari, ifike mahali wasomi wajielewe kama huyu. Utakuta kaKatibu tu wa afya au ka afisa utumishi kanamsumbua mtu na maelimu yake. IT HAS TO STOP. Wasomi wengine mjiongeze na nyie.

Mshahara mdg halafu kero za hapa na pale...huwez kuamini mpk diwani anamkemea mganga mkuu...[emoji15] [emoji15] [emoji15] yn diwan anataka naye awe bosi wako na mipango yote ya kihospitali ipitishwe na vikao vyao vya kata mxiuuu...
tena diwani ambaye kaishia la saba[emoji13] [emoji13] [emoji13]
Nchi hii
 
Huyu dr shimelwa achunguzwe nilishangaa anapata wapi pesa za kununua magari ya kifahari kama vile Range rover na Suzuki tena zero kilometa kutoka cfao motors yeye kama mtumishi wa umma atuambie pesa hizi amezitoa wapi
 
Ninamfahamu ni mwajibikaji, ana jiamini . Sekta ya Afya ni stepping stone ya wanasiasa wengi, hususan kwa kipindi hiki ambacho kila mmoja anataka aonekane amefanya kitu kwa wananchi. Ni uamuzi as busara unapotoa nafasi kwa watakao fanya kwa ubora.
 
Aondoke na achunguzwe kama kweli kaacha bila sababu.
Aende ambako hakuna monitoring.
Analeta vitisho vya kijinga sasa ngoja tuone...!

Labda kama habari hii si ya kweli...
 
Physician aliyesoma na kufanya kazi Germany hashindwi kuwa na Gari hizo, pia ana clinic yake. CFAO wanakopesha magari kupitia bank yako. Stanbic
 
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Dr.Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo na kufuatiliwa kila mara na vyombo vya dola, kasema ni heri afanye shughuli zake binafsi kwa uhuru kuliko hivi ilivyokuwa.
ASEME KWELI UFISADI PESA YA BURE HAKUNA ANATYAKIWA KUFANYA KAZI APATE MSHAHARA.
Mh Rais Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Amesema mashinikizo, siyo kukaguliwa!.

Dr. Anashinikizwa kufanya kazi kama watakavyo wasio kuwa na taaluma. Taaluma inathamani sana.

Engineer, anashinikizwa kujenga miundo mbinu duni ili mradi finishing ing'ae. Muungwana ataona dhamira yake inamshitaki kwa madhara yatakayotokana na kazi yake, na hivyo akiona shinikizo hlio lisiol utaalamu linaendelea, ataachia ngazi. Huo ndio utamaduni tunataka. Lakini isje kuwa yeye ndiye anafanya kazi chini ya kiwango na anataka kuhalalisha kwa sababu zake binafsi. Huyo tutamwambia aende tu.

Hakimu binadamu, vile vile hatakubali kulazimishwa kupindisha hukumu kinyume cha sheria kwa kuwafurahisha watu wasio wana taaluma. Tuliona wa Nkurunzinza, aliondoka usiku kwa usiku na kuenda ukimbizini, akikimbia dhambi ya kupindisha sheria ili zimfae mtawala.

Huo ndio uungwana wa kitaaluma.

Dr. Ahsante kama umeilinda taaluma kwa ustawi wa Afya zetu. Kama umejiuzulu kwa sababu unataka kutetea na kuhalaisha uzembe, uende salama.

Tabby,

Huyo daktari sidhani kama kaamua kuachia ngazi kwa sbb ya kutetea uzembe

Mimi naamini kabisa sababu ya kufanya kazi kwa mashinikizo na pasipo hata kujengewa mazingira bora ya kuifanya kazi yako kwa ufanisi, ndiyo sababu halisi iliyosababisha awaachie kazi yao!!

Naweza kuthibitisha hili pasipo shaka yoyote kwa sababu mimi hapa nilipo ni mtumishi wa umma na kwa sasa kwa kweli tuliochini tunafanya kazi ktk mazingira magumu na dhariri sana hasa kutoka kwa wanasiasa hawa wa kuteuliwa!!

Yaani kuna wengine wanatoa matamko na maagizo yasiyotekelezeka kisheria na kitaalamu ili mradi tu waonekane wamesema na wao ndiyo wakubwa especially hawa wanaoitwa ma DC & RC.....ni shida tupu!!

Mbaya zaidi kwa sasa serikali hai fund kwa kiwango cha kutosheleza taasisi zake karibu zote lakini wakati huohuo wanataka mambo yaende tu!!

Amini usiamini kuna watu ambao hata huwajibiki kwao lakini wanaweza kuja ktk ofisi yako mara leta hili mara kile na mara ifikapo siku flani utuletee hiki na hiki.

Hiyo pengine siyo ishu kubwa sana. Lililo baya zaidi ni kuwa usiseme kuna kitu kimeshindwa kufanyika kwa sababu ya ukosefu wa fedha au kwa sbb ya changamoto hii na hii....wataona wewe ndiye UKUTA....wanalala na wewe mbereeeee!!

Wanachotaka wao ni kuwa wakikuambia paa, usiulize utapaaje wakati wewe siyo ndege mwenye mabawa........wanachotaka wao ni lazima upae tu!!

Dokta yuko sahihi na after all taaluma yake tu ni bidhaa inayojiuza yenyewe!!
 
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Dr.Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo na kufuatiliwa kila mara na vyombo vya dola, kasema ni heri afanye shughuli zake binafsi kwa uhuru kuliko hivi ilivyokuwa.
Hatudanganyiki subirini sio siku nyingi kisutu inamuhusu
 
Ni utaratibu adimu kwa watanzania kujiwajibisha, kama ni kweli kajiuzulu tuangalie kwa mitizamo yote yaani hasi na chanya
 
Back
Top Bottom