Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Tetesi: Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya Amana dr Shimwela amejivua madaraka

Mganga mkuu kachoka yani kila kukicha mara kaja mkuu wa wilaya hajakaa vizuri kavamia waziri hajakaa vizuri mara kaja katibu, hajakaa vizuri kaja Makonda na makamera.
hii nchi kila mtu anajifanya anahusika na kila kitu.
Hili ukweli linakera sana,wakat hao watu wanakuja ukiwaeleza changamoto za hapo kituo cha kazi hawazitatui...........Wiki hii hapo Muhimbili kile kipimo chao kimeharibika tena......kisa kimeelemewa nadhan ni MRI (kama sijakosea)😵
 
Huyo ni doctor mbabaishaji tu. Maana angekuwa mtendaji mzuri asingejivua. Ukanjanja wake umefikia mwisho.
Mzee Abdul Jumbe alijivua nyadhifa zake zote kutoka urais hadi uchama,,,,je alikuwa mbabaishaji?sema Tanzania haijazoea kuskia au kuona watu wakiamua kuwajibika........
 
Mganga mkuu kachoka yani kila kukicha mara kaja mkuu wa wilaya hajakaa vizuri kavamia waziri hajakaa vizuri mara kaja katibu, hajakaa vizuri kaja Makonda na makamera.
hii nchi kila mtu anajifanya anahusika na kila kitu.

Huyu kafungua njia kwa wengine..kuna rafiki yangu ni Katibu Mkuu aliniambia anataka kuchukua hatua kama hii ili arudi zake ughaibuni kufyagia barabara kwa uhuru kuliko kufanya kazi na awamu hii
 
Bora aondoke,wasomi Kibao hawana kazi
Ajira moja hiyo ipo wazi.
Amana Hospital kwenyewe kila siku majanga tu,inaonekana amejitumbua mwenyewe.
Alizoea kufanyakazi kwa mazoea,na kama yupo above 45yrs basi ni muda wa kaachia,damu changa zichukue ajira.
mkuu acha porojo, kuwa daktari sio mchezo
 
Big up daktari, ifike mahali wasomi wajielewe kama huyu. Utakuta kaKatibu tu wa afya au ka afisa utumishi kanamsumbua mtu na maelimu yake. IT HAS TO STOP. Wasomi wengine mjiongeze na nyie.
IT HAS TO STOP!🙁
 
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Dr.Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo na kufuatiliwa kila mara na vyombo vya dola, kasema ni heri afanye shughuli zake binafsi kwa uhuru kuliko hivi ilivyokuwa.
wengi wanaonekana kuegemea upande mmoja bila kuwa na uhakika hasa mashinikizo hayo ni yapi .... then kupata na taarifa ya upande huo mwingne unaolalamikiwa .....

THE FACT OF ANY ISSUE IS WHEN A STORY IS BALANCED FROM BOTH SIDES CONCERNED
 
TumainiEL anataka kutuaminisha kuwa jamaa huyu (dokta) kaacha kazi kwa sababu ya labda eti ni mwizi au kwa lugha ya CCM fisadi!!

Anashindwa kuelewa kuwa, si rahisi mwizi kuachia taasisi aliyokuwa anaiongoza kwa sbb kwa kufanya vile anakuwa amefungua njia ya kuchunguzwa na kisha kushtakiwa.

Mtu anayeacha kazi kwa 24hrs notice, huyo anajiamini....huyo ni clean!!
 
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Dr.Shimwela amejivua madaraka hayo na kuacha kazi ndani ya masaa 24 baada ya kuchoshwa na kufanya kazi kwa mashinikizo na kufuatiliwa kila mara na vyombo vya dola, kasema ni heri afanye shughuli zake binafsi kwa uhuru kuliko hivi ilivyokuwa.
Ni jambo la kusikitisha kwa daktari kuacha kazi.Kusomea udaktari inachukua miaka mingi hadi kuanza kufanyakazi .Nashangaa watu wanatuma msg kama kitu alichofanya daktari ni kitu chepesi.Naomba wanasiasa punguzeni mihemko ili wataalamu wetu wafanyekazi ama sivyo mambo yatazorota.
 
Tuache unafiki madaktari na manesi Huduma zao Ni mbovu hivyo usimamizi WA Katibu unahitajika. Kama yy hapati guess ya kupiga deal asilete visingizio
Unajua wapo wangapi na wanatakiwa wangapi nchi hii au unaropoka tu.
 
Hii kazi wakubwa wakiendelea kushinikiza watu kwa matakwa yao wengi watamwaga!!Taaluma imeingiliwa na wanasiasa!!Ieleweke kuwa taaluma ni kitu kingine na siasa ni kitu kingine!!Wanasiasa waacheni wana taaluma wafanye kazi yao.
 
Mganga mkuu kachoka yani kila kukicha mara kaja mkuu wa wilaya hajakaa vizuri kavamia waziri hajakaa vizuri mara kaja katibu, hajakaa vizuri kaja Makonda na makamera.
hii nchi kila mtu anajifanya anahusika na kila kitu.
kila mtu keshakuwa kambale ndani ya taifa letu.
 
Atupishe tu sasa na vyeti vyake feki maana hakuna namna.
 
Back
Top Bottom