1. Si lazima iwe ni uamuzi unaotokana na mshtuko (panic move/decision). Kwa nini isiwe pia ni uamuzi tu uliopangiliwa vyema baada ya kutafakari vya kutosha? Kwanini isiwe hivyo mkubwa?
Nakuambia hivyo kwa sababu mimi hapa nilishawahi kuacha kazi kwa notice ya masaa 24 ktk taasisi ya moja ya kibinafsi iliyokuwa inanilipa vyema lakini tukashindwa kuelewana na boss ktk maeneo kadhaa.
Na kabla, nilitafakari kwa muda wa takribani miezi miwili hivi, nikajiandaa na kuandaa mazingira kabla ya kuchukua uamuzi rasmi hasa baada ya kujiridhisha kuwa hata nikiacha kazi hii maisha yataendelea tu na kweli yaliendelea hadi leo tena to the best!!
2. Kwani huyu tunayeambiwa kuwa katoa 24hrs notice ya kuacha kazi si daktari? Hana hiyo private clinic na connections hizo zingine ulizozitaja?
Mkubwa, kama tetesi hii ya daktari huyu kuacha kazi ni ya kweli, basi elewa kuwa hakuna lolote la ajabu hapo wala la kushangaa. Hayo mengine tunayodhani ni hivi au vile amini usiamini ni zile zile siasa za wakati huu!!
Yeye hawezi kuwa wa kwanza na wala hawezi kuwa wa mwisho kuchukua maamuzi kama hayo. He is a free person with his own decision ktk kutafuta hali bora zaidi kinafsi na kihali!!
Trust me, kama kawachia kazi yao basi maisha hayasimami yataendelea tu popote atakapo kuwa!!
Ni kweli kabisa ukiona mtu ameamua kuacha kazi kwa hiyari kutokana na majungu ujue huyo mtu ni Innocent kabisa.
Na mara nyingi watu wenye fitina ni wabaya sana. Kuna mtu anaweza akaanzisha majungu tu kwa sababu anafahamiana na wakubwa . Kazi yake ikawa ni kuwafitini wenzake ofisini kwa mambo yasiyo na ukweli.
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kukutwa na sakata kama hilo lakini aliendelea na kazi japo alirushiwa tuhuma na wale waliokua wanapiga dili kutokana na ukweli kwamba yeye alikataa kuungana nao na wala hakuwa kwenye nafasi ya kupiga hizo dili . Hofu yao ikikua kwamba mabadiliko yakitolea yeya ndio ataachiwa ofisi na wao watatolewa au kuhamishwa kitengo.
Walichofanya wale wapiga dili ambao walikua wanashirikiana na wakubwa ni kumpiga fitina ili atolewe maeneo yale au ahamishiwe mbali. Waliunda mkakakati na kuchanga mamilioni na kuibukia wizarani kwa waroho wa fedha ili ionekane kuwa kuna tuhuma na watu wanasambaratishwa kwenye ile idara. Matokeo yake walioondolewa ni wale wasio husika na wahusika waliendelea kupiga dili zao kisayansi na kujifanya kuwa wao ni wema na wabaya wameondolewa.
Tanzania hatutafaulu kuzima wizi ,ufisadi na dili za maofisini bila kuunda tume ya watu waadilifu na kutunga sheria ya kusajili mali zote zilizopo nchini ili wamiliki wake wajulikane na ni kwa namna gani walivyozipata?
Haiwezekani mtoto wa miaka 10 amiliki ghorofa au awe mkurugenzi wa kampuni.
Vinginevyo tujue tu kuwa ni kila zama na kitabu chake. Walituibia wanajibadilisha tu majina lakini ni wale wale.Rasilimali za nchi hii bado iko mikononi mwa wezi. Majumba, mashamba,viwanja na biashara yote haya yanamilikiwa na nani na kwa nini wafikia mahali pa hata kuficha hela kwenye mapipa?
Kwa nini wasijitoe kwenye utumishi wa umma na kuanzosha viwanda na makampuni yao ili angalau watoe ajira kwa watu wengine?
Kwa nini wanaendelea kujimilikisha na maofisi ya umma ilihali wameiba kwa miaka nenda miaka rudi?
Je, hivi ni kweli waliobaki maofisini na kwenye idara mbalimbali ni watu safi au ni kwasababu wanauwezo wa kuwasingizia wenzao waliokosa nafasi za kupenyeza malalamiko yao kwa wakubwa?
Mbona bado waovu wameshikilia maofisi kwa kujibadili tu sura za nje lakini ndani ni wale wale waliojaa uroho na fitina za kila namna!!
Dunia hii haina haki zaidi ya dhulma ,visasi,
Fitina, majungu ,kulogana na kujuana.
Tumeona wale waliokuwa wanachachamaa kuwatukana baadhi ya wanasiasa kuwa wanaukaribu na matajiri na kuwa hela wanazotoa sadaka wanazipata wapi ,leo hii ndio hao hao wanakuwa karibu na makampuni yenye kutia mashaka na wakimimina misaada kwenye taasisi za dini na kuto mahela kama zawadi kila kukicha.
Dawa ya hizi sarakasi ni kutenganisha Kazi za utumishi wa umma na biashara za moja kwa moja. Kama mtu anaona biashara inalipa basi afanye biashara. Kama anataka kutumikia wananchi basi ajitoe kuwatumikia kwa moyo mmoja.