Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Makubi: Wananchi chukueni tahadhari za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa, msisubiri matamko

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Makubi: Wananchi chukueni tahadhari za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa, msisubiri matamko

Acheni wananchi wafe mtajifunza kwa ujinga wenu
Nadhani kwa ujinga wa watanzania walio wengi wa kushikiwa akili kuna njia ngumu twapaswa kuzipata ili tupate fahamu na kujitambua kama hii ya COVID na nyingine nyingi km Carl Marx alivyoishi kuandika.

Jamii ya wajinga wengi hudangwanywa na maneno matamu ya watawala na watu maarufu ktk jamii yao.kwa mujibu wa Carl Marks lazima wakutane na magumu mengi, dhiki na taabu zizalishwazo na wanaoamini ikiwemo vifo, magonjwa, ukosefu wa huduma za msingi za kijamii, ikiwemo chakula, tiba, elimu duni, kuonewa, kudharauliwa,umasikini uliotopea n.k.

Madhila haya yakiwagusa moja kwa moja wataitafuta na kuijua kweli, watamtafuta na kumjua adui yao na watachukua hatua. Tofauti na ilivyo sasa watu wanaishi kwa imani, kwa kuaminishwa kesho iliyo nzuri yaja na kweli wanasubiri, kuna kizazi kisicho na subira chaja,kisicho na uvumilivu, subira wala simile, kisichitaka shida na taabu, kisichoamini ktk nadharia ya kesho. kitaamua hatma yao, na mara nyingi maamuzi hayo hayanaga ustaarabu wala busara.
 
Dah. serikali inaogopa kutamka jina la ugonjwa kama vile inaamini inaweza kuwa “uchuro” au “mkosi” kwa taifa! Tushakuwa na silika za kishirikina!
 
Tutajiongeza wale wenye uelewa, wale watanzania ambao wanasubiri serikali iseme hao inakuwaje?
Kuna ambao mpaka leo wanasema kuwa Magufuli kawashtukia mabeberu, hakuna Korona nchini ni fiksi tu

Hili ndilo neno. Wenye uelewa hatuna shida. Wananchi wa kawaida (the masses) wanaosubiri kauli na maelekezo ya viongozi wapendwa hao ndio wenye hasara.

Juzi kuna kituo cha tv kilikuwa kikihoji watu kadhaa nafikiri mjini Mwanza kuhusu kutovaa barakoa kwenye watu wengi. Majibu ya wengi yalikuwa: “wamesema Tanzania hakuna corona”! Mtangazaji akiuliza “nani kasema?”, watu wazima wanajiumauma tu.

Serikali itimize wajibu kwa wananchi. Kudai watu wasisubiri matamko ndipo wajikinge ni kauli ya reja reja ya kukwepa wajibu.

Tanzania bado ni nchi yenye watu wengi ambao ni masikini wenye uelewa mdogo sana. Hawa wanahitaji “engagement” kubwa ya serikali katika kupigania afya zao. Wanahitaji taarifa sahihi zilizokamilika (detailed) na maelekezo kamili. Kutaka kujibizana na sie tulioko mitandaoni pekee kwa malengo ya kisiasa haisaidii taifa kwa ujumla.
 
Ama kweli awamu hii hatuna viongozi wajibikaji. Kama kuna hatari mbele yetu serikali inaona au haioni? Serikali inasubiri nini kutoa kauli kama kuna hatari au la? Lakini kwanini ikitokea mtu kutangaza "hatari" kama yule mganga wa Chunya anawajibishwa kwamba hana mamlaka?

Mnataka kila mtu afanye kwa namna yake mwenyewe kukabiliana na hatari na si kufuata maelekezo kana kwamba hakuna serkali yenye jukumu la kulinda raia wake.....! Nyie akina Abel kazi yenu ni nini sasa ikiwa kila raia ajiongoze mwenyewe? Mnatuvuruga kwa kweli.
 
Heshima kwako Mganga Mkuu. Hayo yote sisi Wahenga tumeyajua tangu enzi za ujana wetu. Kwa sasa tatizo tulilonalo, hutaki hata kuligusia wala hata kulieleza. Hebu pitia taarifa yako na lifanyie marekebisho.
 
Kuijua serikali na kuilewa hii serikali yetu lazima uwe chizi maana huyu anasema hivi yule vile dah tabu tupu..

Angel naomba nyinge afu uchukue moja uje na bili kabisa
 
Heshima kwako Mganga Mkuu. Hayo yote sisi Wahenga tumeyajua tangu enzi za ujana wetu. Kwa sasa tatizo tulilonalo, hutaki hata kuligusia wala hata kulieleza. Hebu pitia taarifa yako na lifanyie marekebisho.
Bora we so called porofesa kurudi nyumbani ukawapikie mke na watoto! Umeacha kuongelea tatizo la msingi unabaki kujitafuna tafuna mifomo! Yaani mtu mmoja ameigeuza Tanzania imekuwa na watu mazwamazwa kama hawakwenda shule! Shame on you so called mganga mkuu, hustahili hicho cheo!
 
Back
Top Bottom