Acheni wananchi wafe mtajifunza kwa ujinga wenu
Nadhani kwa ujinga wa watanzania walio wengi wa kushikiwa akili kuna njia ngumu twapaswa kuzipata ili tupate fahamu na kujitambua kama hii ya COVID na nyingine nyingi km Carl Marx alivyoishi kuandika.
Jamii ya wajinga wengi hudangwanywa na maneno matamu ya watawala na watu maarufu ktk jamii yao.kwa mujibu wa Carl Marks lazima wakutane na magumu mengi, dhiki na taabu zizalishwazo na wanaoamini ikiwemo vifo, magonjwa, ukosefu wa huduma za msingi za kijamii, ikiwemo chakula, tiba, elimu duni, kuonewa, kudharauliwa,umasikini uliotopea n.k.
Madhila haya yakiwagusa moja kwa moja wataitafuta na kuijua kweli, watamtafuta na kumjua adui yao na watachukua hatua. Tofauti na ilivyo sasa watu wanaishi kwa imani, kwa kuaminishwa kesho iliyo nzuri yaja na kweli wanasubiri, kuna kizazi kisicho na subira chaja,kisicho na uvumilivu, subira wala simile, kisichitaka shida na taabu, kisichoamini ktk nadharia ya kesho. kitaamua hatma yao, na mara nyingi maamuzi hayo hayanaga ustaarabu wala busara.