Mganga wa jadi adai yeye ndiye aliyemuua Nabii T. B Joshua

Mganga wa jadi adai yeye ndiye aliyemuua Nabii T. B Joshua

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mganga wa jadi kutoka nchini Ghana anayefahamika kwa jina la Nana Kwaku Bonsam amedai yeye ndiye anayehusika na kifo cha Nabii maarufu T. B Joshua baada ya mganga huyo kumtuhumu T. B. Joshua kuhusika na kifo cha Rais wa Ghana.

Kwenye video ambayo ameirusha mganga huyo leo, anaonekana akisema kuwa alituma taarifa kwa Papa kuwa ana mpango wa kumuua Nabii huyo.

Nana amesema amefurahi sana kulipiza kisasi cha rais wa Taifa lake. Anasema alimsginda T. B Joshua kwenye Vita yao ya kiroho iliyokuwa nzito sana.
_____________________________________________

I KILLED PROPHET TB JOSHUA..NANA KWAKU BONSAM CLAIMS
-------------------------------------------------
Ghanaian most powerful spiritualist,Dr Nana Kwaku Bonsam, says he killed Popular Nigerian Prophet ,TB Joshua, because the man of God was attacking him in the spirit after he accused him(TB Joshua) of killing Ghanaian President.

In his recent video, posted today, the spiritualist claims to have also reported TB Joshua to the Roman Catholic Pope in Roma for permission to kill TB Joshua.

Nana Kwaku Bonsam says he is happy to have revenged the death of his president by killing the man of God Prophet TB Joshua.

Nana Kwaku Bonsam has been fighting Prophets, Pastors and many men of God from Nigeria accusing them of being liars, deceivers and using magic to perform miracles in the name of God to enrich themselves.
VIDEO: I killed TB Joshua - Powerful Ghanaian traditionalist Kwaku Bonsam provides proof
 
kimenuka kumenuka
Hi niliitabiri siku ile kafa T. B Joshua

Screenshot_20210609-083919.png
 
Familia ya Mo Dewji ikatangaza 1B kwa atakayetoa taarifa za kupatikana mpendwa wao, ikaja ikaongeza dau.

Hawa waganga na manabii sijui walikua wapi kuvuta ule mpunga. Kisha Poo akasema tu huyu atarudi kabla ya J2 na akarudi kweli maajabu yake eti watu hawamuamini Poo kama ni nabii na mchungaji.
 
Tupo tunaangalia katuni moja hapa na wanangu, naona matambiko, ibada za miungu, nk vinaonyeshwa kikatuni ila vina ukweli mkubwa. wazungu walirejea kwenye imani zao za asili baada ya kutupumbaza tukaharibu za kwetu ambazo vilikuwa bora zaidi ya zile za kwao.

Turudi kwenye mada, huyu sio "mchawi" ni muumini wa miungu yetu ya asili yenye nguvu za haraka Sana...TB Joshua alirusha kombora kwa padre wa Ghana naye akajibu kwa nguvu ile ile, hiyo ndiyo nguvu ya Karma!
 
Ni kweli kuwa ukiua kwa upanga nawe utauawa kwa upanga.
Tujikumbushe Bwana Yesu alipo ambiwa na wanafunzi wake wale waliotoka kwa Yakobo na Yohana kwamba ashushe moto ili aangamize, jibu lake lilikuwa je?
.
Luka 9:54-56
[54]Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
[55]Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
[56]Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Yapaswa tujifunze kwa Bwana Yesu. Hatupaswi kuanzisha vita ya kuangamiza roho/nafsi ya mtu mwingine maana hilo sii kusudi la Yesu.
Katika ulimwengu wa roho adui ndie huchokoza na hupenda kuvamia ngome ya mpinzani ama ni kwa Mungu au ni kwa shetani.
Kwa upande wa Mungu yeye Kristo anatufundisha kumwombea adui mema dhidi ya ubaya wake ndipo basi kufanya hivyo huifanya vita iwe ni ya Bwana.
Kinyume cha hilo sii vita ya Bwana bali yenu wanadamu itakayo ongozwa na husuda. Matokeo yake ni kwamba mwenye kumwahi mwezie ni mshindi katika hii vita ya husuda na wote wawili mna hatia mbele za Mungu.
Huyu mganga/mchawi huenda anatafuta kiki au labda kuna ukweli. Kikubwa kwake ni tambo ya kutaka kupanua soko maana nijuavyo mimi kwa mkwara wake huu atapata wateja wengi mno hasa waliopo kwenye madaraka. Baadhi yao hawa watakuwa ni wale waliokuwa wateja wa TB Joshua (r.i.p) waliokuwa wakimpelekea fedha, heshina na vito vya thamani vikimfanya nabii tajiri sana miongoni mwa matajiri wa dunia hii ya leo.
Kanuni ipo wazi na kamwe haipingiki.
"MTENDA HUTENDWA".

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Mganga wa jadi kutoka nchini Ghana anayefahamika kwa jina la Nana Kwaku Bonsam amedai yeye ndiye anayehusika na kifo cha Nabii maarufu T. B Joshua baada ya mganga huyo kumtuhumu T. B. Joshua kuhusika na kifo cha Rais wa Ghana.

Kwenye video ambayo ameirusha mganga huyo leo, anaonekana akisema kuwa alituma taarifa kwa Papa kuwa ana mpango wa kumuua Nabii huyo.

Nana amesema amefurahi sana kulipiza kisasi cha rais wa Taifa lake. Anasema alimsginda T. B Joshua kwenye Vita yao ya kiroho iliyokuwa nzito sana.

VIDEO: I killed TB Joshua - Powerful Ghanaian traditionalist Kwaku Bonsam provides proof
STUPID
 
Back
Top Bottom