Ni kweli kuwa ukiua kwa upanga nawe utauawa kwa upanga.
Tujikumbushe Bwana Yesu alipo ambiwa na wanafunzi wake wale waliotoka kwa Yakobo na Yohana kwamba ashushe moto ili aangamize, jibu lake lilikuwa je?
.
Luka 9:54-56
[54]Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
[55]Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
[56]Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Yapaswa tujifunze kwa Bwana Yesu. Hatupaswi kuanzisha vita ya kuangamiza roho/nafsi ya mtu mwingine maana hilo sii kusudi la Yesu.
Katika ulimwengu wa roho adui ndie huchokoza na hupenda kuvamia ngome ya mpinzani ama ni kwa Mungu au ni kwa shetani.
Kwa upande wa Mungu yeye Kristo anatufundisha kumwombea adui mema dhidi ya ubaya wake ndipo basi kufanya hivyo huifanya vita iwe ni ya Bwana.
Kinyume cha hilo sii vita ya Bwana bali yenu wanadamu itakayo ongozwa na husuda. Matokeo yake ni kwamba mwenye kumwahi mwezie ni mshindi katika hii vita ya husuda na wote wawili mna hatia mbele za Mungu.
Huyu mganga/mchawi huenda anatafuta kiki au labda kuna ukweli. Kikubwa kwake ni tambo ya kutaka kupanua soko maana nijuavyo mimi kwa mkwara wake huu atapata wateja wengi mno hasa waliopo kwenye madaraka. Baadhi yao hawa watakuwa ni wale waliokuwa wateja wa TB Joshua (r.i.p) waliokuwa wakimpelekea fedha, heshina na vito vya thamani vikimfanya nabii tajiri sana miongoni mwa matajiri wa dunia hii ya leo.
Kanuni ipo wazi na kamwe haipingiki.
"MTENDA HUTENDWA".
Sent from my Infinix X622 using
JamiiForums mobile app