Mganga wa kienyeji mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mteja wake

Mganga wa kienyeji mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mteja wake

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia kijana mmoja anayedaiwa kuwa mganga wa kienyeji kwa tuhuma za kumbaka mwanamke aliyekuwa mteja wake katika Wilaya ya Mtwara.

Mtuhumiwa huyo ametambulika kwa jina la Shafii Rashid, mwenye umri wa miaka 23 na mkazi wa Kijiji cha Nanguruwe.

Anatuhumiwa kumfanyia kitendo hicho mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30 (jina limehifadhiwa), ambaye alifika kwake kupata huduma za kitiba.

Tukio hilo linadaiwa kutokea mnamo Septemba 14, 2026, ndani ya nyumba ya mhanga iliyopo katika Kata ya Ziwani, Wilaya na Mkoa wa Mtwara.

Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi, mtuhumiwa alitumia hila kwa kumshawishi na kumwaminisha mwanamke huyo kuwa angepatia dawa maalum ya kutatua changamoto za kiafya zilizokuwa zikimsumbua mtoto wake.

Baada ya kufika nyumbani kwa mwanamke huyo chini ya kigezo cha kumpa matibabu hayo, mtuhumiwa anadaiwa kutumia fursa hiyo kumfanyia kitendo cha ubakaji.

Polisi wanaendelea kumshikilia Shafii Rashid kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kisheria kabla ya kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
View attachment 3673121
Huko kuamini sana waganga wa kienyeji ndiyo mwanzo wa kupeleka UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa majumbani mwao.
NB;Huyo mwanamke angenogewa asingesema wala kulalamika.
 
Back
Top Bottom