Mgao ujao wa umeme…

Tangu Magufuli ameondoka basi kila kitu kimekuwa hovyo tu.
 
Kila hitilafu ikitokea inakuwa oh...fulani angekewepo isingetokea!!
Hata mashine zinachoka na kuhitaji ukarabati...
"Mpaka mvua ikichelewa kunyesha itasemwa kwa kuwa fulani hayupo.."
Tusubiri wahusika watujulishe sababu ya mgao na sio kuangalia nani yupo nani kaondoka...
 
Hadi mwaka jana, inakadiriwa kuwa uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya taifa ulikuwa 1,604MW, huku mahitaji kwenye grid yalikuwa 1,180MW...

Sasa ikitokea chanzo kimoja kikubwa kimezimwa, ndipo hapo upungufu unapojitokeza...

Kitu ambacho nadhani Waafrika kimekuwa kikitukwamisha, ni kutojua au kutilia maanani vipaumbele...

1604MW, kiwango hiki ni chini ya matarajio ya sera ya nishati, ambayo ilikadiria kuwa hadi kufikia 2020, Tanzania ingekuwa ikizalisha si chini ya 5,000MW za umeme kwenye gridi ya taifa, hasa baada ya ugunduzi wa gesi asilia...

Huu ndio ule wakati Waziri Muhongo na wanasiasa wengine walijigamba kuwa mgao wa umeme kuwa historia Tanzania...

Kwa mujibu wa takwimu, matumizi ya bomba kubwa la gesi lile la (Mtwara <> Dar) ni asilimia 6 tu, huku asilimia 94 zikiwa hazitumiki...

Iwapo bomba hilo lingetumika kwa uwezo wake kwa angalau asilimia 50 tu, lingesaidia kuongeza umeme wa uhakika...
 
Kuna Muda Natamani hata nisingezaliwa Tanzania
Unaweza kupata uraia wa nchi yeyote unayotaka si lazima uwe mzaliwa wa hapo.....
Kama kuwa Mtanzania kunakukera badilisha uraia hujachelewa
 
Kwa nini hawana mitambo ya ziada?

Miaka 60 ya uhuru bado tunahangaika na migao ya umeme tu!
 
Hiyo mitambo haikufanyiwa marekebisho kwa muda mrefu sababu wahusika waliogopa kutumbuliwa (hili waziri alishasema)

Sababu za mgao ni kufanya ukarabati na bila kufanya huo ukarabati kipindi hiki huenda hata huo umeme wa mgao usiwepo.....hivyo Watanzania ondoeni wasiwasi kwani hayo matengenezo ni muhimu kipindi hiki.
 
Nakuelewa sana mkuu, wanashatuona wajinga.
"Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?"
 
Nafikiri kwa muda mrefu Tanesco wamekuwa wakiendesha hiyo mitambo bila periodic maintenance kwa kuhofia kuonekana saboteurs baada ya serikali kuahidi hamna mgao. Now the chickens have come home to roost maana wakizidi kuiendesha ita collapse kabisa. Hawana jinsi bali wafanye the long over due maintenance.

Amandla...
 
Subiri subirini kidogo bado tunamalizia keki ya birthday tukimaliza tuhudhurie kongamano moja,teuzi kidogo na semina elekezi tumalizie na birthday ya pinda .Tukimaliza tutaangalia angalia nafasi ikiwepo tutajadili hili swala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…