Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Inadaiwa mgao wa umeme unakuja. Inadaiwa unaanza tarehe 1 mwezi ujao wa Februari.
Sababu ya huo mgao eti ni matengenezo ya mitambo yao ya wapi wapi huko sijui…
Sasa kwa akili zangu hizi za kidato cha nne, ni kama vile sielewi elewi.
Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?
Au zipo? Kama zipo, basi sawa. Ila kwa nchi nizijuazo mimi, kamwe hata mara moja sijawahi sikia eti kutakuwepo na mgao au migao ya umeme kwa sababu mitambo ya kuzalisha au kusambaza umeme inafanyiwa ukarabati.
Hao wenzetu wao mitambo yao huwa haihitaji ukarabati? Kama huwa inahitaji ukarabati, wanawezaje kuepuka migao ya umeme?
Kwa nini sisi kila mitambo inapohitaji ukarabati [ kama ni kweli inahitaji huo ukarabati] basi kunakuwepo na mgao?
Manake hili si jambo geni. Limekuwepo siku zote. Sasa miaka yote hii hawa watu hawajaweza tu kubuni namna ya kuikarabati hiyo mitambo bila kuleta usumbufu wa migao?
Tanesco….and whoever else involved….seriously????
Uko sahihi kabisa. Nimewahi kuishi kwenye taifa moja la magharibi kwa miongo kadhaa, lakini sikuwahi kusikia hicho kituko!
Hata huyo Ma-rope mwenyewe anajua hicho ni kituko, kwa sababu amewahi kuishi Marekani.