Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Salaam ndugu,
Ni hatari kwa afya kumaliza wiki nzima bila kupata maji. Labda sijui walitangaza kutakuwa na mgao wa maji, lakini hakuna mgao unaokwenda mpaka wiki nzima bila maji kutoka. Tunajipa matumaini labda maji yatatoka usiku lakini wapi!
Nilitegemea mvua nyingi zilizonyesha hivi karibuni zingetatua shida ya uhaba wa maji kwa muda mrefu, lakini hiki kinachoendelea kimenishangaza sana.
Hata kama kungekuwa na hitilafu kubwa labda bomba kubwa kupasuka nk, ndio lisirekebishwe wiki nzima?
DAWASA sisi wananchi wa huku tunawalilia, hali ni mbaya sana. Wengine maji ya chumvi ambayo ndio yanuzwa sana mtaani kwa sasa hatuyawezi. Tunataka maji tuendelee na shughuli zetu. Sasa hivi hata kwenda chooni unajipimia ili kubana matumizi ya maji. Kuna jirani yangu mtoto wa mama karudi kwao kisa mtaani hakuna maji.