King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Lakini hapa ilikuwaje Gadner akaruhusu mali zote ziandikwe jina la Jide?? Halafu Gadner si alikuwa anafanya kazi Clouds fm/Times Fm na analipwa Mshahara?? Ina maana hela zote alikuwa anaweka kwenye kapu la Jide?? halafu watu mbona hawajishugulishi kuhoji zilipo mali za Gadner??
Hapo kwenye red... kama Jide alijenga nyumba kabla ya ndoa, kiuhalali ni yake na siyo ya GH. Sio swala la JD kusema mahakamani vithibitisho vitaonyesha
kwenye green: Usajili wa kampuni na assets za Machozi band na MOG restaurant ndio zitatoa muongozo kuhusu mali za hizo kampuni. kampuni inasimama kama separate entity. Mali za kampuni (pamoja na magari) zinabaki kuwa za kampuni siyo za jide. Swali ni kwamba, je GH naye ni mmiliki halali wa kampuni ili aendelee kufaidika na faida itakayokuwa inatengenezwa na kampuni
Kwa ufupi, ndio maana celebrities wa US na Europe wengi huwa wanaoa celebrities wenzao ili kuondoa hii habari ya mtu kuoa/kuolewa na celebrity ili achume mali. Mkiwa wote mpo vizuri kipesa kama Beyonce na Jay Z, Beckham na Posh, mkivunja mkataba kwenye mgao kila mtu inakula kwake. Ni risk kwa celebrity kuolewa na mtu asiyekuwa na pesa
Ni mtizamo wangu tu
Hapo mwanamke ndo angefanyiwa hivi kama anavyofanyiwa gardner humu pasingekalika
gadner arudi kwa mke wake wa kwanza wakagawane mali alizo chuma wakiwa wote aking'ang'ania za jide anatia aibu nani hajui alimkuta jide na mali zake utakoma kaka jipange komando jide kile kichwa hhh hati zote kwa jina la demu hunachako hapo bro anza kuchuma vyako.
kashaolewa hana khabari na ana good life gadner hana maana yule na hawakua na chochote
Kichwa cha nyumba bila pesa? ni ngumu mno. Enzi bible inaandikwa, wanaume walikuwa bread earners so automatically walikuwa vichwa vya nyumba. Hawa wanaume wa sasa wamesahau majukumu ya utafutaji na kuhudumia familia, ni ngumu sana kuwa father house
Haaaahaaa hapo ndipo naamini wanawake ni ajabu la 8 la Dunia maana zingekua mali zina jina la Garder ungeona mashirika ya kupigania haki za wanawake na mikelele yao nashindwa kuelewa inashindikana vipi Garder yeye kupata haki yake siamini kua toka 2005 mpaka leo almost 9-10 years kua jamaa hana mchango kwenye mali za familia yao ni wapuuzi wachache wataamini kua jamaa hana mchango mbona sisi tunagawana tukiwaacha tena mke ni mama wa nyumbani lakini tunathamini mchango wa kulea watoto tu ifike wakati kilio cha haki sawa au 50/50 mkielewe kwa undani kwa tuishio uku Mbwinde ngumu kuelewa ila watoto wa mjini wanajua sacrifies ya Garder kwenye upatikanaji wa mali hizo.
Kumuambia G aanze upya ni kudharau jasho lake kwa miaka 9 naamini Jide anakwepa ngumi ya uso kwa kufumba macho.
Kabla ya kumlaumu Garder tujiulize kama tukivaa viatu vyake tunaweza kutembea navyo hata km 1.
"Don judge a man till u walk a mile in his shoes"
Lakini hapa ilikuwaje Gadner akaruhusu mali zote ziandikwe jina la Jide?? Halafu Gadner si alikuwa anafanya kazi Clouds fm/Times Fm na analipwa Mshahara?? Ina maana hela zote alikuwa anaweka kwenye kapu la Jide?? halafu watu mbona hawajishugulishi kuhoji zilipo mali za Gadner??
Kwa nini asiwe nazo? amekuwa mtangazaji wa Clouds kwa miaka zaidi ya 7 Amekuwa jingles za kutosha tu amekuwa meneja wa wasanii kadhaa hapa town unataka kusema huku pote hakuchuma mkwanja kabisaa??? halafu juzi kati hapa inasemekana kavuta mzigo punda haruki pale EFM aaahh Mbona Gadner mchakarikaji mzuri tuu huu mkwanja wote anaupeleka wapiii???
Gadner naye aache uchizi mimi pia naamini mali ni za Jide , hakuna mwanaume ambaye atanunua magari,kiwanja na ajenge nyumba halafu vyote aandike jina la mke wake, wanaume ni wabnafsi sana.Jide kwahapo namsifu alikuwa mjanja sana.
Gadner atafute hela akaanze maisha aache kulilia mali za mwanamke, yani mali za Jide zigawanywe halafu Gadner akatanue na mwanamke mwingine aha hapana sikubali. Hapa Jide akaze buti hasikubali