HALI tete !
Gardner anataka mgawo wake, lakini sasa utata ulioibuka ni kwamba, inaonekana kama
mali zote ni za Jide kwa vile zimeandikwa majina yake hivyo jamaa ana wasiwasi kwamba Jide anaweza kusema mahakamani
kuwa alizichuma mali hizo kabla ya ndoa , kilisema chanzo hicho kilicho jirani na familia hiyo .
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, utata huo umemfanya Gardner kuwa bize ili kuhakikisha anaumaliza hususan kwenye
nyumba yao iliyopo Mbezi ambapo wengi wanaamini ilijengwa kwa kutumia fedha ya Jide kabla hawajafunga ndoa .
MALI ZINAZOTAJWA
Mali zinazotajwa kuibua utata ni Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni, Dar ambao hivi karibuni Jide aliubadili jina na
kuuita M .O . G Restaurant . Mgahawa huo walipangishwa na mtu.Gari aina ya Range Rover Evoque linalomilikiwa na Judith Wambura Lady Jaydee .
Kuna madai kwamba, Jide na Gardner kabla ya ndoa yao kuparaganyika walikwenda kwa
mmiliki huyo na kusema wameamua kuuacha baada ya mkataba wao kumalizika . Lakini kilichoonekana baadaye, Jide alirudi kwa njia
ya uani na kuanzisha mkataba mpya bila Gardner na kuuita M. O .G .
Mali nyingine mbali na nyumba na mgahawa ni mabasi madogo mawili aina ya Toyota Hiace , moja la Machozi Band na la M .O .G Restaurant . Mabasi hayo yameandikwa Lady Jaydee & Machozi Band .
Hata hivyo , yapo madai kwamba Machozi Band nayo imebadilishwa jina, sasa inaitwa Lady Jaydee
& The Band .
Mali nyingine ni Albamu zote za Jide alizotoa tangu mwaka 2005 wakiwa tayari kwenye ndoa ambapo kwa kawaida mauzo yake ni
endelevu na gari la kutembelea aina ya Range Rover Vogue .
Albamu hizo ni Moto ( 2005) , Shukrani, The Best of Lady Jaydee ( 2006 ) na Nothing But the Truth ( 2014 ) .