Mgao wa Umeme, IPTL, Kinyerezi IV, na Pan African Energy Tanzania (PAET) Ltd: Kwa nini tunarudia makosa ya enzi za Rais Kikwete?

Mgao wa Umeme, IPTL, Kinyerezi IV, na Pan African Energy Tanzania (PAET) Ltd: Kwa nini tunarudia makosa ya enzi za Rais Kikwete?

Habari mkuu
Nadhani Mama Dr.SSH hajapewa taarifa juu ya huu ufisadi. Naomba washauri wa mama wampe taarifa na wampe ushauri stahiki wa jinsi ya kuushughulikia huu ufisadi.
Ahsante
Hata akipewa taarifa hii, kama ni kweli, hakuna hatakachofanya....

Kwan unazan mama hajui kama hamna mgao wa umeme, n hatua gan amefanya yeye kama rais
 
Uzuri wake tunaisoma number wote umeme unakatika kote kote Hadi nyumba za makada wao freshhhh tu twendeni hivi hivi na mvua aitonyesha mwaka huu
 
Hii ni aibu kubwa kwa nchi kama Tanzania kukosa umeme, yenye vyanzo vingi vyakuzalisha umeme wananchi inabidi tujaribu kubadirisha viongozi,wanaongoza wameshindwa
 
Sisiem na ile cartel ya Pablo Escobar hawana tofauti, tofauti nchi tu

Ni uharamia na ufisadi kwa kwenda mbele.
 
View attachment 2758556
Mhe. Doto Biteko , Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Tangazo la serikali kuhusu mgao wa umeme unaoendelea limekuja wakati ambapo kuna maswali mengi juu ya kusimamishwa kwa Mradi wa Umeme wa Kinyerezi IV.

Pia limekuja wakati ambapo kuna harakati za serikali kununua umeme kutoka kwenye kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd (PAET), yeye vinu vyake huko kusini mwa Tanzania. Kampuni ya PAET ni kama IPTL.

Hadi 2015 kampuni ya IPTL ilimilikiwa na Mechmar pamoja na VIP Engineering. Kwa mujibu wa mkataba wa miaka 15, baada ya 2015 umiliki wa IPTL ulitakiwa uhamie serikalini.

Miaka 2 kabla ya muda wa mkataba kuisha, ikulu ya Tanzania chini ya Rais Kikwete iliuza IPTL kwa Singh Habinder wa PAP na kuwawezesha kina Singh kupata access ya pesa kwenye account ya Escrow pale Benki Kuu.Nao kina Singh waligawana na kubeba pesa taslim kutoka Stanbic Bank.

Sasa kampuni ya Pan-African Energy iko inazalisha umeme ili kuiuzia serikali kama ilivyokuwa inafanya IPTL. Mradi wa Kinyerezi IV umesitishwa ili kutengeneza uhaba wa umeme na hivyo Pan-African Energy kupata uhalali wa kuiuzia serikali umeme.

Wapiga dili na madalali wa kuuza nchi walioshuhudiwa katika enzi za Kikwete wamerudi ikulu!

Lengai Ole Sabaya pamoja na matatizo yake yote aliwahi kuongea juu ya hili kama ifuatavyo:
Nachukia kuwa mtanzania Kwa kasi sana

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom