Michuano yote ya caf pesa zinalipwa mpaka mashindano yaishe.
Ikitokea timu haina pesa za kujiandaa basi ni mpaka labda ibembeleze ipewe hela za usafiri na chakula na malazi lakini hio pesa itakatwa kwenye pesa kamili itayopewa mashindano yakiisha.
Wabongo wengi lugha ni changamoto kufuatilia vyanzo official vya CAF na inakuwa rahisi wachambuzi kuaminisha uongo, nakumbuka ni hawa hawa wachambuzi walidanganya kwamba timu zinachukua pesa za kufuzu hatua ya makundi, robo fainali, nusu fainali, fainali, ubingwa wakati utaratibu haupo hivyo.
Na hio ya kila timu kupewa pesa za maandalizi tofauti na zilizopangwa kwenye bajeti ni stori za wachambuzi zisizo na ushahidi ama zilikuwa ni tetesi, kama sio weka ushahidi wa caf