Mgawanyo wa Mamlaka: Ni sahihi IGP kuthibitisha usalama wa Chanjo, Tiba au dawa fulani?

Mgawanyo wa Mamlaka: Ni sahihi IGP kuthibitisha usalama wa Chanjo, Tiba au dawa fulani?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali.

Sitaki kuwauliz hawa wote kuwa miaka ya Nyuma wakati Chanjo imepatikana upi ulikuwa msimamo na walisema kitu gani kuwaambia waliotaka Chanjo ije mapema. Tuyaache hayo maana ni vituko tu. Tumesikia kwenye vyombo habari vya kimataifa kuwa kuna mataifa ikiwemo Uingereza ambako watu walichanjwa na baadhi damu ziliganda na kuleta shida. Je hii inafaa kuwahakikishia watanzania kwa nguvu zote kuwa chanjo ni salama 100%. Kwa nini isitolewe na Side effects zake tukajua the risk.

Swali langu kwa wanabodi Je ni vipi kila mwenye Mamlaka anatuambia Dawa hii ni sahihi ama dawa ile si sahii, mathalan chanjo hii ni sahii ama ile si sahihi. Nimetoka kumsikia IGP akituambia kuwa chanjo hiyo ni salama na inafaa kwa sisi kuchanjwa. Je kisheria imekaaje?.

Je ni kwamba anasapoti msimamo wa Nani na amethibitishaje maneno ya kina Vibwetere kuwa ni ya Uwongo?.. kama ni wa Serikali ni serikali ya awamu ipi?
 
Banana republic. Kila mmoja anajaribu kumjibu Ngwajima Kibwetere
 
Ndipo ujue hizi chanjo ni siasa laghai

Kwa mara ya kwanza naunga mkono hoja ya Membe.
Kwa nyongeza yeyote mwenye nguvu hii ya kubadilisha misimamo iwe ya mtu ama ya serkali atuambie uhakika wake juu ya matokeo ya hiki kinachcoitwa chanjo ya corona ambacho anayechanjwa bado anaweza kuambukizwa ama kuambukiza corona...
Kampatie mama yako
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali...
Hapa niacheni nicheke tu nikalale zngu🤣🤣🤣
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali.... kama ni wa Serikali ni serikali ya awamu ipi?
Usalama wa taifa ndio Wana mamlaka ya kuthibitisha usalama wa chanjo kabla haijatumika Kwa wananchi
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali... kama ni wa Serikali ni serikali ya awamu ipi?

Hili suala la chanjo limeanika kwa uwazi jinsi tunavyoongozwa na viongozi wajinga na walinda matumbo. Leo hii akiingia rais atakayepinga hiyo chanjo, hawa wote wanaosifia sasa wataioinga pia.
 
Anahakikisha ulinzi na usalama.
usalama ni wa kila kitu
 
Hili suala la chanjo limeanika kwa uwazi jinsi tunavyoongozwa na viongozi wajinga na walinda matumbo. Leo hii akiingia rais atakayepinga hiyo chanjo, hawa wote wanaosifia sasa wataioinga pia.
Mayinyi wapinzani msimamo wenu ni upi!!!!

Mnachanjwa nao au hamchanjwi!!!
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali... kama ni wa Serikali ni serikali ya awamu ipi?
Ukiishasikia kiongozi wa umma,tafsiri yake ni hiyo.

Maana yake,anachoongea na anachotenda ndicho kinafaa kufatwa.
Kama kina walakini hapo ndipo imani ya serikali nzima kwa wananchi huyeyuka au kufubaa.
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali.. kama ni wa Serikali ni serikali ya awamu ipi?
JF imeshuka hadhi sana. Ni kwa sababi imevamiwa na watu kama wewe. Ulichoandika wala hakileti sense yoyote. Moderators, mngetutendea haki sana kama mngeanzisha jukwaa la siasa ka lugha ya kiingereza. Hilo jukwaa litachuja uchafu kama huu.
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali... kama ni wa Serikali ni serikali ya awamu ipi?
Chanjo zote tulochanjwa huweki signature yako, ila unapewa cheti tu.

Kwanini hii ya corona inabidi uweke sahihi yako?
 
Inabidi watuweke wazi.

Huu ni msimamo wa nani?
Na wa Before ulikuwa wa nani.?

Isije tokea yalitokea then tukashft again.!
 
Hata Mimi ninashangaa Sana .hii hutokea tanzania pekee Askari kutumika kisiasa badala ya kulinda
 
Nikiacha tamko la IGP kuwa tuwapuuze wale wanaopinga kuchanjwa Covid ambao Mh. Waziri wa Afya amewaita Vibwetere, Azim Dewji akiwashambulia kuwa wanaingilia fani zao na kwenda Mbali zaidi kwa UVCCM na baadhi ya wabunge kuwashambulia kwa maneno mbalimbali...
Heading na Content haviendani
 
Kwani yale yaliyosemwa mwanzo na serikali hii hii kuhusu chanjo yamekwishafanyiwa kazi? Tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom