Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.

Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana

Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha

Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu

Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane

Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee

Cc Wizara ya Afya Tanzania


Asante TANESCO kwa majibu mazuri ya mipango ya kupambana na shida ya umeme ya muda mfupi na muda mrefu.
Sisi wananchi tunafarijika sana mnaposikia sauti zetu na kutujibu kama hivi
Ila sasa mjitahidi kwenda na hiyo mipango kwa wakati ili mwakani muda kama huu kukawa na tatizo hilihili na majibu yakawa hayahaya

Plan nzuri bila utekelezaji makini na kwa wakati inakua mbaya zaidi kwa wananchi waliokua na subra, Rais amewaamini abajua nyie ni wataalamu mnaoweza kumsaidia kuwahudumia watu wake. Basi msiipoteze imani ya watanzania kwa serikali yao

Tanesco Kazi iendelee 👍

 
Huyo mama yenu kila siku yeye anahujumiwa tu!!

Hawezi kubeba majukumu ya Urais na kutenda kazi inavyompasa?

Amebweteka tu na maushungi hawajibiki zaidi ya kulalamika anahujumiwa?

Ni nani anayemuhujumu? Acheni USANII nyie.

Nchi imewashinda mnajificha kwenye visingizio uchwara. Ati anahujumiwa!
 
Hujuma dhidi ya Samia zimekuwa nyingi tena ni haohao Wanaccm wenzake wameanza kampeni.
Acheni USANII nyie wababaishaji tu hamna lolote.

Taasisi zote ziko chini ya Rais na serikali yake! Kama kweli anahujumiwa kwanini asiwawajibishe hao wahujumu?

Urongo mtupu! Mwambieni ukweli huyo mama kwamba hajiwezi, acheni kulaghai watu eti anahujumiwa!

Anajihujumu mwenyewe na udhaifu wake!
 
Huyo mama yenu kila siku yeye anahujumiwa tu!!

Hawezi kubeba majukumu ya Urais na kutenda kazi inavyompasa...
Hii comment sio ya kupuuza, hii ndio picha wanayopewa watanzania kuhusu serikali yao, na ujumbe uwafikie
#WaziriMwenyeDhamanaYaUmeme
#WaziriMwenyeDhamanaYaMaji
#IdaraZoteZinazohusika

Sisi wananchi tunasema mama yetu Samia anza kuwashughulika wote wanaoshindwa kuhudumia wananchi. Tumbua mama uteue walio tayari kufanya kazi usiku na mchana kuondoa hizi kero ndogondogo kwa wananchi
 
Muda wa Asali huu na Maendeleo binafsi ya watu.

Hayo ma umeme na maji ni maendeleo ya vitu, na maendeleo ya vitu aliondoka nayo mwendazake.

Tafta channel ya asali ununue jenereta lako, uchimbe kisima chako uache malalamiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…