Mgawo wa Umeme wasitishwa, utafiti mpya umeona hauhitajiki kama awali

Akiwa bungeni, Naibu waziri wa Nishati, Byabato ametangaza kusitisha mgao uliotangazwa awali kwa madai kwamba hauhitajiki baada ya kufanya utafiti huku wakiwa wamepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia kwamba mgao usiwe mkali kama ilivyotangazwa.

Si walisema ni matengenezo?

Sasa imekuwaje tena?. Walipochepusha ndo ikajitengenezo hiyo mitambo?
 
Leo mpaka Unguja mgao umehathiri saloon yangu hapa Utapoa daa, jirani yangu juice imedoda ahahaaaa...
 
Hii nchi bure kabisa...., Kwahio mgao sio kwamba hakuna jinsi (yaani last option) ni kwamba ni uamuzi wa mtu kuamua makali yake yanakuwaje (yaani anaagiza uwe mkali kidogo) Kwanini asiagize usiwepo kabisa ?

Na hapo Makamba anafanya nini, Kwanini hizo njia zinazotumika sasa zisingetumika kuanzia miezi kadhaa iliyopita ? Kwahio bila kupokea maelekezo wenyewe wangekata tu....
 
Sisi leo wametoa ratiba ngoma inakata kianzia saa 2:00 mpaka saa 6 usiku na wamekara hapa hatuna umeme ni upuuzi huu
 
DRAMA nyingi sana. Mpaka Rais aseme ndo mawaziri wabadilike na kutosumbua raia.
 
Akiwa bungeni, Naibu waziri wa Nishati, Byabato ametangaza kusitisha mgao uliotangazwa awali kwa madai kwamba hauhitajiki baada ya kufanya
Inabidi kuwe na mawasiliano kati ya serikali na watendaji wake. Inakuaje mtendaji atoe tamko halafu serikaki ibatilishe. Ina maana kila mtu anafanya kazi kivyake. Kuwe na mawasikiano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…