Upuuzi uliopo kwenye soka la bongo ambao Ulaya sijawahi kuusikia:
1. Mgeni rasmi. Tena mwanasiasa ambaye ni kiongozi wa chama
2. Msemaji wa timu kuwa maarufu kuliko hata kocha, baadhi ya wachezaji, nk. Msimu ule Mbeya kwanza ikiwa ligi kuu (nadhani msimu mmoja ama miwili iliyopita) nilikuwa namfahamu msemaji/admin wa timu hiyo nikiwa simfahamu mtu mwingine yeyote pale! Yaani nilikuwa najua jina la timu na la msemaji/admin pekee! Jamaa alikuwa akiongea sana na mitandaoni hakauki.
Sent using
Jamii Forums mobile app