Mgodi wa North Mara imeleta maafa Ziwa Victoria tena, Serikali inajiuma uma tu kwa kamati feki

Mabwawa ya maji ya sumu yamefanyeje!?

Mleta mada sijakuelewa, dadavua, je, umeshawahi kufanya kazi au kuishi huko North Mara?!
 
North Mara ni Barrick Gold? Nakumbuka siku ile Mufti Zuberi alisema Uhuru Stadium kwamba anamuomba Mungu ai Barrick Tanzania.

Naanza kufikiria Samia Suluhu amekalia kuti kavu.
 
Ni wazi kwamba North Mara Gold mine ltd wanatumia pesa kuficha ukweli na kuumiza wananchi na mazingira. Kwa ujumla wananchi wote wa TZ tunaumizwa maana tunakula samaki wa ziwa nchi nzima.
Damu ya wahanga wa hiyo sumu i juu ya waliotenda unyama huo na watoto wao
 
Halafu wasichojua madhara ya kemikali kama hizo ni cumulative hasa linapokuja swala la kusababisha magonjwa ya saratani, huwezi shangaa kuna cases nyingi za magonjwa ya saratani kanda ya ziwa........

huenda hao watu wanaoonyesha dalili sasa walianza kuathirika zaidi ya miaka 10 nyuma..
 
Au ndio maana wengi kule huugua figo
 
Au ndio maana wengi kule huugua figo
Exactly, kwenye nchi zao wapo very strict kwenye kujali afya za raia........huku hawakupi huo uthamani zaidi ya kujali kupata faida nono kwenye makampuni yao, kwa sera ya kujipimia ambayo hangaya aliipigia promo tutarajie wananchi zaidi kuathirika.
 
Nchi hii jifunze vitu ili uone faida yake ipo kwa ajili ya taifa au mtu mmoja mmoja.

Although mambo mengi si kwa ajili ya taifa ni mtu mmoja mmoja, hakuna na hata akiwepo anayesimamia taifa hatakuwa na nguvu ya wapambe sababu wapambe wanataka pesa siyo longolongo.

Acheni yatokee hakuna mwenye kusimamia haya.
 
Kutokuwa makini kwao umekupimaje? Walishapewa kazi kama hii wakaboronga?

Kina nani ambao wako makini ulitamani wawepo kwenye kamati?

Ni mtanzania gani asiependa pesa?
Tatizo liko clear kamati ya nn kama si upigaji tu?
 
Sasa naanza kuelewa kwa nini kanda ya ziwa inaongoza kwenye ugonjwa wa saratani Tanzania.

Ni muhimu uchunguzi wa kina ufanyike....kwenye hii migodi yote Geita, North Mara, Stamigold, Bulyanhulu na Buzwagi sijui wameshafunga na ile ya zamani Buhemba.

Na baadhi zinazoibuka...
 
Yale yale masuala ya minamata bay..hii nchi hii..viongozi ni laana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi najua mgodi haupaswi Kuwa karibu na vyanzo vya maji
 
..serikali sio mbia ktk hiyo kampuni?
Unaonaje matokeo ya Kamati inayosema ni vinyesi vya ng'ombe na maozea ya miti ndo yameleta vifo vya samaki?

Halafu kiongozi wa kamati ni profesa, aliyewahi kupachikwa kuwa Mkemia mkuu wa serikali.
 
Mabwawa ya maji ya sumu yamefanyeje!??
Mleta mada sijakuelewa, dadavua, je, umeshawahi kufanya kazi au kuishi huko North Mara?!
Dah! Una umri gani boss?

Hilo suala linaeleweka duniani na mtetezi mkubwa wa wananchi walikuwa wananchi wa Canada.
 
Dah! Una umri gani boss? Hilo suala linaeleweka duniani na mtetezi mkubwa wa wananchi walikuwa wananchi wa Canada.
Mie kijeba, nina safari za kimachinga huko Nyamongo, Matongo, Kewanja n.k na kulikuwa na mradi WA waste management mkubwa wa gharama kubwa, tailings storage facility’s (TSF) pond.

Siamini zoezi lile linaweza kusababisha uvujaji wa maji ya sumu kuelekea Mara river!
 
Kutokuwa makini kwao umekupimaje? Walishapewa kazi kama hii wakaboronga?

Kina nani ambao wako makini ulitamani wawepo kwenye kamati?

Ni mtanzania gani asiependa pesa?
Vipi?

Unajisikiaje kuuliza swali hili hapo zamani, leo hii umeambiwa ni kinyesi cha ng'ombe?

Nipe sifa kwa kuelewa mambo basi!
 
Maneno matamu sana hayo, tena ya kitaalamu sawa na wachungaji wa ahadi ya mbingu.

Je, Duniani kote uliwahi sikia kinyesi kikileta vifo vya samaki?

Samaki wamo hata ndani ya wastewater!
 
Haijawahi kutokea eti kinyesi na mkojo wa ng'ombe kwenye maji yanayotembea unasababisha sumu ya kuua viumbe walioko majini?

Nilikuwa JKT kwa mwaka mzima, kipindi tunapata mafunzo ya porini tulikuwa tunapitishwa kwenye malambo ya maji ambamo mifugo inakunywa na kujisaidia lakini mpaka tuna maliza mafunzo hakuna hata mmoja aliyeugua typhoid nk iweje sasa eti kwenye mto Mara mifugo imechangia uwepo wa sumu iliyoathiri uhai wa samaki kwenye maji yanayotembea?

Mwenyekiti wa kamati hiyo amefanya uchunguzi kwa faida ya aliyemtukama sio uhalisia na matokeo yakinifu ya kitaalamu-apewe pole kwa kupotosha umma na kama nafsi inamsuta anatakiwa aombe radhi kwa kuwa osio yeye pekee mwenye uwezo wa kuchunguza kisababibisha cha madhara kwa samaki ndani ya maji yanayotembea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…