Mgodi wa Shantamine Chunya unakusanya dhahabu nyingi lakini hauna impact yoyote nchini

Mgodi wa Shantamine Chunya unakusanya dhahabu nyingi lakini hauna impact yoyote nchini

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Nimesafiri Huko chunya mkoani Mbeya kibiashara mara kadhaa kibiashara, kuna mgodi mmoja unakusanya dhahabu balaa lakini hauna impact yoyote kwenye hii nchi. Naomba kuuliza, sio kwa kuusemea ila kiukweli, hivi hawa watu kweli bado wanafanya pembuzi yakinifu au tunapata gawio kiasi gani kila mwaka, mbona sijawahi kusikia? nimejiuliza maswali mengi sana.

1. Mgodi wa Shantamine ni mkubwa na wa zamani sana, ni kweli kwamba hadi leo hawapati faida bado wanapata hasara ili kutupatia mrahaba?

2. Mgodi wa shantamine ni mgodi mkubwa sawa tu na hiyo ya Geita na Kahama, lakini hauvumi.

3. Mgodi wa Shantamine umezungukwa na wachimbaji wadogowadogo ambao wanapata kweli dhahabu, ni kweli kwamba wachimbaji wadogowadogo wanaouza dhahabu hapa soko la dhahabu la Chunya wanaweza kupata dhahabu lakini hao wenye machinery hadi leo bado hawajapata faida ili watupe mgao?

4. Nilishawahi kupita pale airport songwe/mbeya nikakuta mapolisi wametanda kusindikiza ndege iliyobeba madhahabu ya huu mgodi, uliza mtu yeyote mfanyakazi wa shantamine akuambie kama wanapata dhahabu au la na wanapakia dhahabu mbeya airport/songwe au la.

5. Viongozi waandamizi wanafaidika vipi nao, mfano, mgodi unalindwa na mapolisi, Tanzania tunafaidika nao vipi? mapolisi wanalipwa na mgodi. pia, wakuu wao ni kweli wanapata mgao ili kupeleka mapolisi na kuwalinda? kuandia mawaziri, maRPC, wabunge n.k.

Tunataka kujua faida ya huu mgodi, kama hakuna faida basi waachiwe wananchi watanzania wazawa wachimbe kuliko mzungu kuchimba akilindwa na mapolisi wetu halafu anapakia dhahabu kwenye ndege na kuondoka nayo. jambo hili linaweza kupuuzwa ila ni la kwetu. Hakuna uwekezaji, mtu anakuja kuchimba dhahabu ya kwetu hapa nchini anapakia na kwenda nayo halafu tukitaka mgao anasema hajapata faida? je? tunapata mgao kiasi gani? kwa waliofika chunya, kuna dhahabu balaa. wabongo tuchangamke.
 
Ule mgodi unasemekana ni wa kikwete unasimamiwa na ridhiwan

Kuna kipindi fulani ilikua kila jumamosi choppa inatua kuchukua mzigo na kusepa.
hata kama ni wa kikwete, anatoa gawio serikalini au hatoi? though wasimamizi pale ni wazungu, ila unalindwa na mapolisi kabisa wanaenda kwa zamu kama hao wanaoenda bank.
 
Kwanza ujue mrabaha hautozwi kwenye faida. Pili shanta ni mgodi wa kati,a mining licence,ukubwa wa mgodi unakuwa determined na capital investment.

Huwezi kusema mgodi ni mkubwa sababu tu macho yako yameona mchanga mwingi umerundikwa au mataa mengi yanayomeremeta ndani ya mgodi.
 
Kwanza ujue mrabaha hautozwi kwenye faida
Pili shanta ni mgodi wa kati,a mining licence,ukubwa wa mgodi unakuwa determined na capital investment
Huwezi kusema mgodi ni mkubwa sababu tu macho yako yameona mchanga mwingi umerundikwa au mataa mengi yanayomeremeta ndani ya mgodi.
mgodi wa kati unaochimbwa eneo lenye madini nje nje tu (kwa ushuhuda wa wachimbaji wadogowadogo), mapolisi wetu ndio wanawalinda, halafu unasema tumeona mchanga mwingi? mbona wanapakia mawe airport sasa kama hawapati faida?
 
Kwanza ujue mrabaha hautozwi kwenye faida
Pili shanta ni mgodi wa kati,a mining licence,ukubwa wa mgodi unakuwa determined na capital investment
Huwezi kusema mgodi ni mkubwa sababu tu macho yako yameona mchanga mwingi umerundikwa au mataa mengi yanayomeremeta ndani ya mgodi.
kwahiyo faida ya ule mgoni ni nini? kwa watanzania.
 
Nimesafiri Huko chunya mkoani Mbeya kibiashara mara kadhaa kibiashara, kuna mgodi mmoja unakusanya dhahabu balaa lakini hauna impact yoyote kwenye hii nchi. Naomba kuuliza...
Inaonekana unaokoteza manebo ua mitaani badala ya kuitafuta ukweli.

Shanta mine, siyo sawa na Bulyanhulu, Buzwagi, Geita au North Mara.

Mgodi huo wa Shanta mine ni mgodi wa kati, siyo mgodi mkubwa - ni ML (Mining License). Hiyo mingine niliyoitaja ni SML (Special Mining License).

ML - uwekezaji wake si zaidi ya $100m. SML - ni uwekezaji wa zaidi ya $100m.
 
Inaonekana unaokoteza manebo ua mitaani badala ya kuitafuta ukweli.

Shanta mine, siyo sawa na Bulyanhulu, Buzwagi, Geita au North Mara....
kwa dhahabu ile mnapakia airport, kwa mishahara ile mnalipa watumishi, vyakula vile mnalisha watumishi, ni mgodi wa $100ml? basi yapasa tuwapime upya tujue kama mnastahili kuwa hapo au la.
 
mgodi wa kati unaochimbwa eneo lenye madini nje nje tu (kwa ushuhuda wa wachimbaji wadogowadogo), mapolisi wetu ndio wanawalinda, halafu unasema tumeona mchanga mwingi? mbona wanapakia mawe airport sasa kama hawapati faida?
Hata hujaelewa vigezo nilivyoweka kuhusu mgodi kuwa mkubwa au wa kati..
Mrabaha hautozwi kwenye faida isipokuwa kwenye gross value
Kuwa muelewa basi
 
Kwanza Shanta haipo Chunya mkuu, Shantamine ipo karibu na Mkwajuni, Saza na Patamela na upo katika wilaya ya Songwe, Katika Mkoa wa Songwe na sio Mbeya.

Pili kuhusu ukubwa ni kweli nadhani Shanta ni wa pili kwa ukubwa Tanzania kama sikosei baada ya GGM. Sijajua ni kwa nini hausikiki kabisa, lazima kuna matatizo sehemu.
 
Hata hujaelewa vigezo nilivyoweka kuhusu mgodi kuwa mkubwa au wa kati..
Mrabaha hautozwi kwenye faida isipokuwa kwenye gross value
Kuwa muelewa basi
OK, hawajafikia kiwango cha kutakiwa kutupatia mrahaba. mtaji wao waliouorodhesha kwenye makaratasi au niseme kwa leseni yao wanatambulika kama mgodi mdogo au wa kati.

Hawatakiwi kutupatia mrahaba. sasa sisi tumeshaona wanapakia sana dhahabu ambayo ni zaidi hata ya huo mtaji wao, maisha yao tu yanaonekana ni zaidi hata ya mtaji wao.

Wafanyakazi wa pale wanatuambia kuna dhahabu kibao inapatikana na wanaiba pia na kuiuza hapa chunya, nenda uliza wafanyabiashara ya dhahabu watakuambia kule chunya.

Mbeya wanapakia dhahabu mara nyingi tu yenye thamani zaidi ya huo mtaji umetaja, je, kuna haja ya kuwatathimini upya au tuendelee kuwachukulia kama wao ni mgodi wa kati? wewe ni mtz?
 
Kwani umeona wapi wamesema hawapati faida?

Umesikia wapi hawatoi mrahaba?

Wanatoa mirahaba kwa jinsi ya stahiki yao. Alafu koma kulinganisha shanta na Geita, sawa?
 
Tunatoza mrabaha,ada ya ukaguzi,service levy ya halmashauri,vat na corporate tax wanapopata faida
Bila kusahau ajira kwa watz na corporate social responsibility.
umesahau na mgao mnaowapatia viongozi waandamizi wa mkoa ili wawasitiri, mbona halmashauri yenyewe hapo mlipo niliona wana hali mbaya, hela wanafanyia nini sasa? mmewapatia kiasi gani mwaka jana?
 
Kwani umeona wapi wamesema hawapati faida?

Umesikia wapi hawatoi mrahaba?

Wanatoa mirahaba kwa jinsi ya stahiki yao. Alafu koma kulinganisha shanta na Geita, sawa?
biashana na jamaa hapo juu amesema hamtakiwi kutoa mrahaba kwasababu ninyi ni mgodi wa kati. najua wengi hapa mna maslahi na shanta, lakini jueni hicho mnachokula ni makombo tu, chakula halisi kinabebwa na wenyewe.
 
OK, hawajafikia kiwango cha kutakiwa kutupatia mrahaba. mtaji wao waliouorodhesha kwenye makaratasi au niseme kwa leseni yao wanatambulika kama mgodi mdogo au wa kati. hawatakiwi kutupatia mrahaba...
Mrabaha wanatozwa na tozo nyingine. Kuwa mgodi wa kati au mkubwa hakuwi determined na kiasi cha dhahabu iliyopo unapochimba,ni initial capital investment ndiyo determinant.

Popote watakapopeleka hiyo dhahabu ndani ya Tanzania wataishia kuiuza kwenye masoko ya dhahabu unless wanasmuggle nje ya nchi ndio tatizo linaweza kuwa.
 
Back
Top Bottom