Mgodi wa Shantamine Chunya unakusanya dhahabu nyingi lakini hauna impact yoyote nchini

Mgodi wa Shantamine Chunya unakusanya dhahabu nyingi lakini hauna impact yoyote nchini

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza,mimi ninafanya kazi SMTL na wanalipa kila kitu kinachotakiwa kama mwekezaji
tufahamishe mzee, wanalipa nini na nini? pale kwenye kamji kenu mbona masikini sana wakati kuna mgodi mkubwa vile? wanatoa mrahaba? au wao ni mgodi wa kati hawatoi? najua hapa maafisa madini watakuja kama mbogo kuupigania kwasababu wana vimigao vidogovidogo hivi vya milioni kadhaa kila mwezi.
 
Mrabaha wanatozwa na tozo nyingine
Kuwa mgodi wa kati au mkubwa hakuwi determined na kiasi cha dhahabu iliyopo unapochimba,ni initial capital investment ndiyo determinant..
Popote watakapopeleka hiyo dhahabu ndani ya Tanzania wataishia kuiuza kwenye masoko ya dhahabu unless wanasmuggle nje ya nchi ndio tatizo linaweza kuwa.
wakipakia dhahabu pale mbeya airport, ni kwamba wanaiuza hapa nchini?
 
umesahau na mgao mnaowapatia viongozi waandamizi wa mkoa ili wawasitiri, mbona halmashauri yenyewe hapo mlipo niliona wana hali mbaya, hela wanafanyia nini sasa? mmewapatia kiasi gani mwaka jana?
You are too emotional..
Mbona kuna mineral auditors pale mgodini hadi strong room
Wanachofanyia halmashauri service levy zao zipo kwenye mipango yao ya halmashauri husika.
 
biashana na jamaa hapo juu amesema hamtakiwi kutoa mrahaba kwasababu ninyi ni mgodi wa kati. najua wengi hapa mna maslahi na shanta, lakini jueni hicho mnachokula ni makombo tu, chakula halisi kinabebwa na wenyewe.
Mimi sibishani na mtu. Nimekujibu wewe kwenye bandiko lako, wewe ndio umesema Shanta wanasema hawapati faida hence hawatoi mrahaba! Na kisha kwa kutokujua kwako ukasema mgodi wa shanta ni sawa na Geita na mingine.
shanta.jpg
 
wakipakia dhahabu pale mbeya airport, ni kwamba wanaiuza hapa nchini?
Ukiona wanapakia pale songwe airport ujue wana clearance zote na washalipa kila kitu
Dhahabu haiondoki bila kuwepo tra,watu wa tume ya madini na vyombo vya ulinzi na usalama
Kama unajua wanaotorosha madini,isaidie nchi yako kwa kutoa taarifa tume ya madini/wizara ya madini.
 
tufahamishe mzee, wanalipa nini na nini? pale kwenye kamji kenu mbona masikini sana wakati kuna mgodi mkubwa vile? wanatoa mrahaba? au wao ni mgodi wa kati hawatoi? najua hapa maafisa madini watakuja kama mbogo kuupigania kwasababu wana vimigao vidogovidogo hivi vya milioni kadhaa kila mwezi.
MGODI MKUBWA KAMA ULE HAUQWEZI KUFANYA UJANJA UJANJA ,WANALIPA KODI ZOTE NA MIRAHABA SERIKALINI ,MKOA WA SONGWE UNANUFAIKA SANA NA MRAHABA NA KODI ZA SERIKALI WANALIPA TRA (LAGER TAX PAYERS)

WANA MAKAMPUNI MAKUBWA YANAYOTOA HUDUMA NA YOTE YANALIPA KODI STAHIKI ,OFISI YAO DAR ES SALAAM NA CHUNYA NDIO MAAFISA WA MADINI NA KODI WANAPOKUJA KUFANYA UKAGUZI MARA KWA MARA
 
Ule mgodi unasemekana ni wa kikwete unasimamiwa na ridhiwan

Kuna kipindi fulani ilikua kila jumamosi choppa inatua kuchukua mzigo na kusepa.
JF imekuwa kama kijiwe cha kahawa sababu ya watu kama wewe. "Insemekana" ni tuhuma, unaweza kuthibitisha? Au unatumika kuchafua watu?
 
JF imekuwa kama kijiwe cha kahawa sababu ya watu kama wewe. "Insemekana" ni tuhuma, unaweza kuthibitisha? Au unatumika kuchafua watu?
Tuhuma na tetesi zote ni habari ambazo hazijawa official verified hata CNN na BBC wanatumia.

Sijamchafua mtu kwasababu habari ipo based kwenye hearsay
 
kwa dhahabu ile mnapakia airport, kwa mishahara ile mnalipa watumishi, vyakula vile mnalisha watumishi, ni mgodi wa $100ml? basi yapasa tuwapime upya tujue kama mnastahili kuwa hapo au la.
Tatizo mnasikiliza maneno ya mtaani, huna uhakika na chochote, unaleta JF.

Unakataa siyo investment ya S100m, kwa hiyo ni investment ya dola ngapi?

Unaelewa maana ya CAPEX? Unaelewa tofauti ya CAPEX na OPEX? Kinachoelezea aina ya leseni, siyo uzalishaji, siyo wali wanaokula wafanyakazi au dhahabu inayopakiwa kwenye ndege au kubebwa kwenye toroli, ni Capital Investment.

Unatakiwa kujielimisha kwenye sekta, inaonekana umepitwa na mengi.
 
Kwanza Shanta haipo Chunya mkuu, Shantamine ipo karibu na Mkwajuni, Saza na Patamela na upo katika wilaya ya Songwe, Katika Mkoa wa Songwe na sio Mbeya.

Pili kuhusu ukubwa ni kweli nadhani Shanta ni wa pili kwa ukubwa Tanzania kama sikosei baada ya GGM. Sijajua ni kwa nini hausikiki kabisa, lazima kuna matatizo sehemu.
Umefika Nyamongo ukaona NORTH MARA GOLD MINING mkuu au kupata taarifa zake.
 
Kwanza Shanta haipo Chunya mkuu, Shantamine ipo karibu na Mkwajuni, Saza na Patamela na upo katika wilaya ya Songwe, Katika Mkoa wa Songwe na sio Mbeya.

Pili kuhusu ukubwa ni kweli nadhani Shanta ni wa pili kwa ukubwa Tanzania kama sikosei baada ya GGM. Sijajua ni kwa nini hausikiki kabisa, lazima kuna matatizo sehemu.
Shanta mine ni mgodi wa kati, siyo mgodi mkubwa. Kwa ukubwa:

1) Geita mine
2) Bulyanhulu
3) North Mara
4) Buzwagi

Hiyo yote ni SML. Shanta mine ni ML.
 
Mkuu, ule mgodi ni mkubwa lakini sio kweli kwamba unalingana na mgodi wa Kahama ama Geita.
Na unaposema wanapata dhahabu nyingi unamaanisha, wanapata ounces ngapi per 1 tone..??
 
OK, hawajafikia kiwango cha kutakiwa kutupatia mrahaba. mtaji wao waliouorodhesha kwenye makaratasi au niseme kwa leseni yao wanatambulika kama mgodi mdogo au wa kati.

Hawatakiwi kutupatia mrahaba. sasa sisi tumeshaona wanapakia sana dhahabu ambayo ni zaidi hata ya huo mtaji wao, maisha yao tu yanaonekana ni zaidi hata ya mtaji wao.

Wafanyakazi wa pale wanatuambia kuna dhahabu kibao inapatikana na wanaiba pia na kuiuza hapa chunya, nenda uliza wafanyabiashara ya dhahabu watakuambia kule chunya.

Mbeya wanapakia dhahabu mara nyingi tu yenye thamani zaidi ya huo mtaji umetaja, je, kuna haja ya kuwatathimini upya au tuendelee kuwachukulia kama wao ni mgodi wa kati? wewe ni mtz?
Wewe unaokoteza maneno ya mitaani. Kwa sheria ya Tanzania, hakuna anayezalisha dhahabu bila kulipa mrabaha, inspenction ja local levy (7.3% on gross). Mrabaha unalipwa kila unapozalisha, uwe unapata faida au faida. Hivyo Shantamine, kama walivyo wachimbaji wengine, wanalipa mrabaha, inspection fee ja local levy kila wanapozalisha.

Kinacholipwa ukianza kupata faida ni corporate tax (30% on net profit).
 
Hakuna mgodi unaopata hasara nchini hizo ni lugha za kibiashara tu Kama unapata hasara mbona ufungi.
Mkuu, kwanza mleta mada hajazungumzia swala la Shanta Mine kupata hasara.
Pili, migodi (dhahabu) ni biashara kama biashara zingine na hivyo basi hasara ni sehem ya biashara na hutokea kwenye migodi pia.
Ukisema mbona hawaondoki, manayake kwangu inanipa jibu rahisi kwamba bado haujui lolote kuhusu migodi/dhahabu ama biashara.
Kwakifupi ni kwamba, mtu anapo wekeza fedha nyingi kwenyw biashara flani na akawa anapata faida, then ikatokea biashara ile ikayumba kidogo na akajikuta anapata hasara, hii haimaanishi basi kwamba aondoke. Kumbuka hapo kabla alikua anapata faida na pia amewekeza mtaji mkubwa pamoja na kujenga miundo mbinu.
 
Kwanza ujue mrabaha hautozwi kwenye faida. Pili shanta ni mgodi wa kati,a mining licence,ukubwa wa mgodi unakuwa determined na capital investment.

Huwezi kusema mgodi ni mkubwa sababu tu macho yako yameona mchanga mwingi umerundikwa au mataa mengi yanayomeremeta ndani ya mgodi.
Huwezi kupima mgodi ukubwa kulingana na uzalishaji wake? Wanaweza weka mtaji mdogo lakini wakazalisha dhahabu nyingi kuliko migodi 'mikubwa' ya kanda ya ziwa.
 
Back
Top Bottom