Mgodi wa Shantamine Chunya unakusanya dhahabu nyingi lakini hauna impact yoyote nchini

Mgodi wa Shantamine Chunya unakusanya dhahabu nyingi lakini hauna impact yoyote nchini

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza,mimi ninafanya kazi SMTL na wanalipa kila kitu kinachotakiwa kama mwekezaji
Mkuu ebu tuambie, ni kweli mgodi unamilikiwa naa Kikwete? Kwa kuwa unafanya kazi hapo lazima unajua kitu
 
Nimesafiri Huko chunya mkoani Mbeya kibiashara mara kadhaa kibiashara, kuna mgodi mmoja unakusanya dhahabu balaa lakini hauna impact yoyote kwenye hii nchi. Naomba kuuliza, sio kwa kuusemea ila kiukweli, hivi hawa watu kweli bado wanafanya pembuzi yakinifu au tunapata gawio kiasi gani kila mwaka, mbona sijawahi kusikia? nimejiuliza maswali mengi sana.

1. Mgodi wa Shantamine ni mkubwa na wa zamani sana, ni kweli kwamba hadi leo hawapati faida bado wanapata hasara ili kutupatia mrahaba?

2. Mgodi wa shantamine ni mgodi mkubwa sawa tu na hiyo ya Geita na Kahama, lakini hauvumi.

3. Mgodi wa Shantamine umezungukwa na wachimbaji wadogowadogo ambao wanapata kweli dhahabu, ni kweli kwamba wachimbaji wadogowadogo wanaouza dhahabu hapa soko la dhahabu la Chunya wanaweza kupata dhahabu lakini hao wenye machinery hadi leo bado hawajapata faida ili watupe mgao?

4. Nilishawahi kupita pale airport songwe/mbeya nikakuta mapolisi wametanda kusindikiza ndege iliyobeba madhahabu ya huu mgodi, uliza mtu yeyote mfanyakazi wa shantamine akuambie kama wanapata dhahabu au la na wanapakia dhahabu mbeya airport/songwe au la.

5. Viongozi waandamizi wanafaidika vipi nao, mfano, mgodi unalindwa na mapolisi, Tanzania tunafaidika nao vipi? mapolisi wanalipwa na mgodi. pia, wakuu wao ni kweli wanapata mgao ili kupeleka mapolisi na kuwalinda? kuandia mawaziri, maRPC, wabunge n.k.

Tunataka kujua faida ya huu mgodi, kama hakuna faida basi waachiwe wananchi watanzania wazawa wachimbe kuliko mzungu kuchimba akilindwa na mapolisi wetu halafu anapakia dhahabu kwenye ndege na kuondoka nayo. jambo hili linaweza kupuuzwa ila ni la kwetu. Hakuna uwekezaji, mtu anakuja kuchimba dhahabu ya kwetu hapa nchini anapakia na kwenda nayo halafu tukitaka mgao anasema hajapata faida? je? tunapata mgao kiasi gani? kwa waliofika chunya, kuna dhahabu balaa. wabongo tuchangamke.
Mkuu mmiliki wa Shanta mine ni mangi. Huwa Wana akili ya kudeal na waziri husika , wanamalizana juu kwa juu. Huko ikungi singida, bado wananchi wanapigwa risasi kila siku anamiliki ikungi yote.
 
Chalamila alikua RC wa mkoa Mbeya, inakuaje ukamwona "akiweka mambo sawa" kwenye mkoa mwingine (Mgodi upo mkoani Songwe).

Ukisema ulimwona kabla mkoa wa Mbeya haujagawanywa, swali langu litakuja kwako kwamba ulimwona akifanya hivyo angali ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa ?
(Chalamila kawa RC wa Mbeya baada ya kugawanywa).
Naomba ufafanuzi wa ulichokiona mkuu
Kwani Chunya ina mgodi huo tuu? Mbona soko la madini limejengwa Chunya badala ya huko Songwe?
 
Masoko ya madini ya serikali yapo ktk wilaya karibu zote zinazozalusha madini ikiwamo Songwe na Chunya, sasa sinui nani alikuambia kuwa Sobgwe hakuna soko? Nenda Mkwajuni utaluona soko mkuu.
 
*Dhahabu nyingi
*Mgodi mkubwa

umepimaje?
Umelinganisha na nini/mgodi gani?
 
Back
Top Bottom