Mkuu, kwanza mleta mada hajazungumzia swala la Shanta Mine kupata hasara.
Pili, migodi (dhahabu) ni biashara kama biashara zingine na hivyo basi hasara ni sehem ya biashara na hutokea kwenye migodi pia.
Ukisema mbona hawaondoki, manayake kwangu inanipa jibu rahisi kwamba bado haujui lolote kuhusu migodi/dhahabu ama biashara.
Kwakifupi ni kwamba, mtu anapo wekeza fedha nyingi kwenyw biashara flani na akawa anapata faida, then ikatokea biashara ile ikayumba kidogo na akajikuta anapata hasara, hii haimaanishi basi kwamba aondoke. Kumbuka hapo kabla alikua anapata faida na pia amewekeza mtaji mkubwa pamoja na kujenga miundo mbinu.